Diterbitkan 2:19:00 PM
Na Mwandishi wetu-Utouh News
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetakiwa kurekebisha Sheria ya kanuni ya adhabu na Sheria ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji ,uhaini na ugaidi.
Hayo yamejiri jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya siku ya kupinga adhabu ya kifo duniani yenye kauli mbiu isemayo ''umaskini na haki ni mchanganyiko hatari''.
Akizungumza na wanahabari Mratibu wa Dawati la Katiba wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ANNA HENGA amesema kuwa wanapinga adhabu ya kifo kwa sababu ni adhabu ya kibaguzi na kikatili inayotweza utu wa binadamu.
"tunapenda kuweka wazi kwamba hatukubaliani kwa namna yeyote na vitendo vya mauaji na tusingependa kuona muuwaji anauwawa baada ya kuua,kufanya hivyo ni kuhalalisha kifo",alisema Henga.
Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt JOHN MAGUFULI kwa kuweka wazi msimamo wake wa kutokuunga mkono adhabu ya kifo kwani ni adhabu ya kinyama na isiyomstahili binadamu yeyote Yule.
Takwimu zinaonyesha mpaka kufikia mwaka 2015 kulikuwa na jumla ya watu 472 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa ambao kati yao 452 ni wanaume na 20 ni wanawake.
0 maoni:
Chapisha Maoni