WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 10 Oktoba 2017

 04:42      No comments

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe Bwn.Haji Mnasi akizungumza na waandishi wa Habari alipofika katika kuhudhuria mkutano wa 33 wa jumuiya ya serikali za mitaa(ALAT)

                                    Na Joseph lieme

Mkutano wa 33  Jumuiya  ya Serikali za mitaa Tanzania ( ALAT)  leo umeanza rasmi jijini Dar es salaam  , ambapo Meya wa jiji la Dar es salaam isaya Mwita amewapokea wajumbe wa mkutano huo kutoka sehem mbalimbali  za mikoa ya Tanzania.

Akizungumza katika  ukaribisho huo Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo ambae pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe Bwn.Haji Mnasi amesema mkutano huo unatarajiwa  kufunguliwa rasmi kesho na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. Dr John Pombe Magufuli ambapo wajumbe hao wataendelea vikao hadi tarehe 6 octoba  kujandili mambo mbali mbali yanayo zikabili serikali za mitaa.

Aidha amesema jumuia hiyoinatarajiwa kuwasilisha maombi rasmi kwa Rais Magufuli ili vyanzo vya mapato vilivyo chukuliwa na serikali kuu viweze kurudishwa katika  Halmashauri iliziweze kuongeza uwezo wa kujiendesha .

Awali akizungumzia maendeleo pamoja na juhudi katika Halmashauri yake nBwn. Mnasi amesema kuwa amejipanga vilivyo hasa katika kuhakikisha kuwa anakuwa mfano wa kuigwa katika utumishi hasa katika kuhakikisha anasimamia vyema mapato na vyaanzo mbali mbali vilivyopo kwenye halmashauri yake husika 

Sanjari na hayo amewaomba watanzania wote hasa wale waliopo kwenye Halmashauri yake ya wilaya ya Ileje kujumuika pamoja katika kudumisha sekta ya kukubaliana na juhudi za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli pamoja na uadilifu ulio sahihi mbele ya Taifa la Tanzania.

Mkutano huo wa jumuiya ya serikali za mitaa ambao unataraji kuanza kuanzia siku ya leo na tayari wajumbe wote wa mkutano huo wamekwisha wasili Jijini Dar es salaam na wakapokelewa na Meya wa Jiji la Dar es salaam Bwn. Isaya Mwita Na unatarajiwa kufunguliwa rasmi hapo kesho tarehe 03.10.2017 na Rais Magufuli na baadae utachukua hadi tarehe 05.10.2017 ndipo utakapomalizika na wajumbe wote kutoka Tanzania nzima wamekwisha fika na kuhudhuria.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *