Digital Online
Torintohot Media Blog.
Na Dustan Mhilu.
SHULE ya Sheria Tanzania na Shule ya Sheria nchini Uganda zimepanga kuingia makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ili kuboresha utoaji huduma ya kisheria kuanzia ngazi ya kitaaluma hadi katika jamii.
Mazungumzo ya makubaliano hayo yalifanyika jana katika ofisi za shule ya sheria Tanzania iliyopo Sinza Dar es Salaam ambapo ujumbe shule ya sheria kutoka Uganda uliongozwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Profesa Frank Othembi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Makamu Mkuu , Mipango, Fedha na Utawala wa shule ya sheria Tanzania , Profesa Ambrose Kessy alisema mpango huo wa ushirikiano ni matunda ya safari yao ambapo shule ya sheria nchini waliitembelea shule ya sheria Uganda na kujifunza mambo mbalimbali ambapo kwa kiasi kikubwa Uganda wamepiga hatua kwakuwa walianza miaka ya 1970.
“Wenzetu hawa wametutembelea ili kuona ninamna gani twaweza shirikiana katika utoaji wa elimu ya sheria na utoaji wa huduma na msaada wa kisheria ambapo wenzetu wapo mbali zaidi kwakuwa mawakili katika nchi yao hutoa huduma hiyo kwa wasiyoweza kulipa mawakili bure” alisema Profesa kessy.
Sanjari na kauli ya Profesa Kessy kukili kwamba Uganda wamepiga hatua kubwa alijivunia kwa taasisi yake kwakutoa elimu bora na wahitimu mahiri na hivyo kuwataka wanaotaka kujiunga na shule wasisite kwani elimu itolewayo katika taasisi hiyo ni ya viwango vya juu vinavyohimili ushindani wa soko kimataifa.
Vilevile Profesa Kessy alisema kwamba taasisi hiyo ipo katika utekelezaji wa mpango wa Rais Dk, Samia Suluhu Hassa wa msaada wa kisheria ambapo mpango huo huwandaa wasaidizi wa sheria kwa ajili ya kuisadia jamii katika utatuzi wa migogoro,jinai na madai kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa shule ya sheria kutoka Uganda, Frank Othembi alisema kwamba wamekuja Tanzania kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wao kitaaluma ambapo pia wana mpango kuziunganisha shule za sheria za Afrika Mashariki katika mashirikiano ya utoaji huduma za kisheria.
“Tunayo furaha kuwa Tanzania leo (jana) tumepata mapokezi mazuri lakini pia tumeona ni namna gani Tanzania nayo imepiga hatua tumeona maktaba iliyosheheni vitendea kazi ikiwemo vitabu vya kujifuniza vya kiada na ziada na mfumo wa tehama ukifanya kazi vizuri ni matumaini yetu baada ya mazungumzo yetu tutatoka na maazimio ya pamoja katika kuimarisha sekta ya sheria na utoaji haki katika nchi zetu za Afrika Mashariki” alisema Profesa Othembi
0 maoni:
Chapisha Maoni