Digital Online
Torintohot media Blog.
Na Dunstan Mhilu na Joseph Liemi
MENEJIMENTI ya Chuo Kikuu Ardhi imemshukuru Rais Dk, Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwakukiwezesha chuo hicho kuwapatia Sh 67.7 bilioni kupitia mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unaojulikana kwa jina la Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation-HEET).
Hayo yalielezwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa alipozungumza na HabariLEO mwishoni mwa wiki katika viunga vya Chuo hicho mkoani Dar es Salaam.
“Kwanza ni mshukuru Rais Dk, Samia Suluhu Hassan, binafsi nilikuwa nikisema na nnaendelea kusema na kurudia tena kwamba mradi huu mkubwa sana kwetu Chuo Kikuu Ardhi n ani mategemeo yetu kuwa mradi huu utaboresh miundombinu ambayo tulikuwa tuki ihitaji kupanua chuo hususani katika kuongeza programu mpya za mafunzo na udahili wa wanafunzi”
Alisema Prof Liwa.
Kwa mujibu wa Profesa alisema kwamba mradi huo utakapokamilika utawezesha kuwa na mabadiliko katika mitaala ya kufundisha, ongezeko la majengo ya madarasa, maabara, studio na karakana, kuongeza vifaa mbalimbali vitakavyotumika wakati wa kufundisha pamoja na kuongeza kuwajengea uwezo wafanyakazi.
“Ni furaha yangu kuujulisha umma wa Tanzania utekelezaji wa maeneo yote ya mradi wa HEET kwa Chuo Kikuu Ardhi na nita taja kwa mangu kama ifuatavyo”
Kwenye mradi huo chuo kinajenga majengo mapya makubwa manne katika Makao makuu ya chuo hicho eneo Survey Dar es Salam ambayo ni jengo la madarasa, jengo la maabara mtambuka, jengo la studio na jengo la karakana mbalimbali.
“Ninafuraha kusema hadi kufikia Novemba, 2023, ujenzi wa majengo haya kwa ujumla wake ulifikia asilimia 17, majengo haya yatakuwa na uwezo wakuchukuwa jumla ya wanafunzi 5,660 na watumishi 73 haya ni mafaniko makubwa kabisa” alisema Prof Liwa
Kwa upande wa Kampasi mpya ya Mwanza inayojengwa huko Sengerema kwenye eneo la ukubwa wa Ekari 378, tunatarajia kuanza ujenzi wake wa majengo mapya Matano yenye uwezo wakuchukuwa jumla ya wanafunzi 2,132 na watumishi 131, ambapo ujenzi huo utaanza baada ya kukamilika kwa tathimini ya zabuni ambayo inatarajiwa kukamilika katika robo ya pili ya mwaka.
0 maoni:
Chapisha Maoni