Na Mwandishi wetu.
November 21, 2023
Akizungumza jijini Dar es salaam mwenyekiti wa machifu hapa nchini Chifu Antonia Sangalali ambaye pia ni mjumbe wa kamati amesema matembezi hayo ya amani yanaatarajiwa kufanyika Novemba 25 mwaka huu ambapo yatahusisha viongozi mbalimbali wa dini pamoja na watanzania wote wenye mapenzi mema na Taifa.
Jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania JMAT inatarajia kufanya matembezi makubwa ya amani yenye lenfgola kupongeza kazi zinazofanywa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania
Akizungumza jijini Dar es salaam mwenyekiti wa machifu hapa nchini Chifu Antonia Sangalali ambaye pia ni mjumbe wa kamati amesema matembezi hayo ya amani yanaatarajiwa kufanyika Novemba 25 mwaka huu ambapo yatahusisha viongozi mbalimbali wa dini pamoja na watanzania wote wenye mapenzi mema na Taifa.
Amesema ni vyema watanzania wakajitokeza katika matembezi hayo kwani kila mmooja anaona yale mazuri yanayofanywa na serikali katika kuendelea kudumisha amani na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo ameongeza kuwa T-Shirt za matembezi hayo pia zinatolewa makao makuu ya jumuiya hiyo jijini Dar es salaam kwa bei ya Tsh 25,000 ambayo kila mtanzania amepewa rai kushiriki matembezi hayo.
Aidha ameongeza kuwa jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania itaendelea kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu kwani amani yetu ni tunu kubwa ya Taifa letu.
Amesema mgeni rasmi katika matembezi hayo anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa Tanzania ,Kasim MAJALIWA
0 maoni:
Chapisha Maoni