Torinto Hot Media Blog.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 22, 2023 ameongoza wadau wa TCC na Chama cha washereheshaji Tanzania na wakazi wa Kigamboni kufanya usafi fukwe ya pweza Wilaya ya Kigamboni ikiwa ni Kampeni ya safisha, Hifadhi Bahari.
Akiongea wakati wa zoezi hilo RC Chalamila ametoa rai kwa wadau wengine kuunga mkono juhudi za safisha, Hifadhi Bahari na kufanya usafi katika maeneo mengine ya Jiji hilo ambapo amekaribisha wadau wenye dhamira ya kuwekeza katika taka kuja kuwekeza.
Aidha Mhe Chalamila ametoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano Mkubwa wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu Rasirimali watu hivyo Jamii na wakazi wote kuendelea kufanya usafi na kuliweka Jiji safi ili kuleta taswira nzuri ya nchi yetu.
Vilevile kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Halima Bulembo amesema Wilaya hiyo ni moja ya Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam yenye fukwe nyingi ambazo ni muhimu katika sekta ya utalii wa fukwe hivyo Kampeni ya safisha Hifadhi Bahari ni muhimu kwa mstakabali wa kuwa na fukwe bora na zinazovutia.
Mwisho Mhe RC amekabidhiwa vifaa mbalimbali vya usafi kama mifagio, pipa la kuhifadhia taka na life Jacket
0 maoni:
Chapisha Maoni