Torinto hot media Blog.
Na Jerome Mlaki wa DAR
December 22, 2022
UTARATIBU wa kwanza, ili kuwa ni kuchoronga na kujenga njia ya kuchepusha maji ya mto ili kupata eneo kavu katikati ya mto lililowezesha kujenga tuta kubwa litakalohifadhi maji na kutoa nafasi kwa Wakandarasi kutekeleza majukumu yao.
UTARATIBU wa pili, waliweza kujenga tuta kuu la kuhifadhi maji yaliyo kuwepo awali ili yasiweze kuingilia au kuleta ghasia wakati wa utekelezaji mkuu wa Ujenzi wa bwawa.
UTARATIBU wa tatu, ni kuchoronga na kujenga njia za kuporomosha maji ili yaweze kuzungusha vinu vya kufua umeme.
UTARATIBU wa nne ni kujenga, kuunga na kusimika mitambo na vinu vya kufua umeme.
UTARATIBU wa tano ni kujenga kituo cha kusafirisha umeme ili uweze kutumika katika gridi ya taifa.
UTARATIBU wa sita ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere mpaka Chalinze ili kuingiza umeme kwenye gridi ya Taifa na kutumiwa na wananchi.
UTARATIBU wa saba ni ujenzi wa daraja la kudumu ambalo linawezesha shughuli mbalimbali za bwawa ziendelee.
UTARATIBU wa nane ni ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi na barabara za ndani ya mradi ambazo ziliwezesha shughuli mbalimbali za upitishaji wa vifaa vya Ujenzi.
#BwawaLetuLaNyerere #HatuaKubwaYaKihistoria #KuelekeaUmemeWaUhakika
0 maoni:
Chapisha Maoni