Na torinto Hot media Blog.
Na Jerome Mlaki wa DAR.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula (kushoto) na Meneja Masoko wa GSM, Rukia Yazid, wakizindua kwa pamoja leo Novemba 10, 2022 Maadhimisho ya Siku ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSD22) yatakayofanyika mwanzoni mwa Desemba. (Picha na Jerome Mlaki).
Taasisi ya sekta binafsi Tanzania inatarajia kuadhimisha siku ya sekta binafsi Tanzania (TPSD22) Ndani ya wiki ya kwanza ya mwezi Desemba 2022 .
Tukio Hilo litafanyika kwenye ukumbi wa The Superdome Arena, Masaki Dar es Salaam, Tanzania.
TPSD22 Imeandaliwa na TPSF Kwa kishirikiana na wadau Muhimu wa sekta binafsi na Wizar ya uwekezaji, viwanda na biasharaili kuenzi na kutambua mchango wa sekta binafsi katika uchumi wa nchi.
Zaidi ya wambe 1000 ambazo ni viongozi wa kisekta,wakurugenzi watendaji, na maafisa waandamizi wa serikali watakussnyika kujadili dhima kuu ya kuimarisha ushindani wa sekta binafsi.
Lengo la tukio hili pia ni kutadhmini mafanikio ya sekta binafsi ktk kipindi Cha Mwaka 2021-2022, huku tukiangazia mazingira Bora ya biashara na uwekezaji ambayo yamechochea ukuaji wa uchumi chini ya uongozi wa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya awamu ya sita. Amesema Bi. Angelina Ngalula.
0 maoni:
Chapisha Maoni