WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 10 Novemba 2022

 03:54      No comments
.

Na Torinto hot Blog.

Jerome Mlaki wa DAR.



Wasanii wa Muziki nchini Tanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kongamano la Muziki la ACCES linaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 24 hadi 26 mwaka huu ili waweze kukutana na wanamuzii wa kimataifa na kubadilishana uzoefu.




Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Hassan Abbas wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema sekta ya sanaa na utamaduni inazidi kukua kutokana na Tanzania kuwa nchi ya 5 Afrika kufanyika kwa Tamasha hilo kubwa linalowahusisha wasanii wakubwa wakimataifa.

TanzaniaTena; Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia jambo hili kubwa Afrika na linalowaleta wadau kutoka Afrika na kote duniani, imedhamini sehemu ya mkutano huu kwa nia ya kuwaletea karibu wasanii wetu fursa za kujua masoko makubwa zaidi na fursa za kujuana. na wakubwa zaidi. Sisi tumetimiza wajibu wetu,” Amesema Dkt. Abbasi.










Kwa upande wake Mkurugenz wa Music in Africa Foundation Eddie Hatitye amesema lengo la mkutano huo na wanamziki ni kukuza vipaji na ubunifu wa wanamuziki, kutangaza na kukuza biashara kwa kukutana na wadau wa kimataifa wenye nia ya kufanya biashara ya mziki.







Aidha ametaja faida nyingine za mkutano huo kuwa ni kutengeneza ushirikiano mpya wa kibiashara, kubadilishana ujuzi na mawazo, kujiunga na mtandao wa wadau muhimu wa Muziki barani Afrika pamoja na kupata maarifa mapya ya kugundua vipaji vipya vya mziki.

“Ni fursa kwa wasanii wa Tanzania kukutana na wadau wa kubwa wa muziki Afrika kama wasanii wenzao, wauzaji kazi za muziki kama Sony, Boomplay na Universal na kwa ujumla ni fursa ya kukua,” Amesema Eddie Hatitye Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Access ya Afrika Kusini inayoratibu mkutano huo kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania.



Naye Katibu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Faridy Kubanda marufu kama Fid Q amesema mkutano huo ni fursa nzuri kwa wanamziki wa Tanzania kujitokeza na kujisajili katika mkutano huo ili waweze kujifunza mbinu mbalimbali za kukuza soko la mziki pamoja na chapa zao.




Hata hivyo amesema kupitia mkutano huo wananii wa Tanzania wataweza kukutana na wanamziki wakubwa wa kimataifa na kubadilishana uzoefu pamoja na kampuni kongwe za muziki duniani ambazo zinauzoefu wa kutosha katika biashara ya mziki Duniani.



“Mi naona mkutano huu unakuja kujibu maswali yetu yote kuhusu vipi tunaupeleka mbele muziki wetu tunakutana vipi na wadau wakubwa Afrika na duniani. Shirikisho la muziki linawaomba wadau wote tujisajili maana ndio sharti la kuhudhuria mkutano huu katika pages za Access kwani ni bure kabisa,” Amesema Msanii Fid Q.


Novemba 24-26 mwaka huu wataalamu na wadau wa muziki Barani Afrika wanakutana Tanzania kwa siku tatu za watu kubadilishana mawazo na maonesho ya muziki wa Afrika na jiji la Dar es Salaam tena katika kumbi za Julius Nyerere (kwa mkutano) na BreakPoint Makumbusho (kwa maonesho ya muziki jioni) linakwenda kuwa mwenyeji wa tano tangu mkutano huo mkubwa uanze kufanyika Afrika.


0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *