Torinto hot media Blog.
Na Jerome Mlaki wa DAR
Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS imshukuru jitihada za Rais Samia katika kuwezesha mazingira bora ya Uwekezaji ambayo yameiwezesha kuvuka malengo ya ukuaji wa mfuko kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wawekezaji toka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa mwaka 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS Simon Migangala amesema jitihada za kukuza uchumi zinazofanywa na serikali zimewezesha UTT AMIS kupitia mifuko yake 6 ya Uwekezaji kuimarika na kuongeza idadi ya wawekezaji.
“Katika taasisi ambazo zimenufaika na jitihada za Rais za kuchochea uwekezaji na sisi UTT AMIS ni mojawapi hivyo tunamshukuru sana Rais Samia kwa jitihada zake za kuiunganisha Tanzania na mataifa mengine jambo ambalo limechoche ongezeko la wawekezaji wa ndani na nje ya nchi “ Amesema Mkurugenzi Migangala.
Aidha amesema mwamko na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu faida zinazotokana na masoko ya fedha, mazingira mazuri ya uwekezaji yenye utulivu wa soko ndio yanayochochea ukuaji mzuri wa mfuko huo
Sambamba na hayo amewataka Watanzania kujiunga na mfuko huo kwani kutokana na utulivo wa soko la uwekezaji wanatarajia mfuko huo kwa mwaka ujao kukua zaidi na kuongeza faida kwa wanachama.
Hatahivyo amesem mfuko uliofanya vizuri vizuri kiuwekezaji kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 ni mfuko wa Bond Fund ukifuatiwa na Liquid Fund, Wekeza Maisha na kumalizia na mfuko wa watoto.
Ametoa wito kwa wajasiriamali kuwekeza katika mfuko huo kidogo kidogo ambapo watapata faida na mtaji wa kukuza biashara zao.
0 maoni:
Chapisha Maoni