WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 1 Novemba 2022

 05:55      No comments

 

Torinto hot media Blog 

Na Jerome Mlaki wa DAR 




Rais Samia Suluhu Hassan akitembelea baadhi ya mabanda katika Kongamano la Kitaifa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia katika ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es es salaam.


Dar es Salaam:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuundwa kwa kikosi kazi kitakacho shughulikia nishati safi ya kupikia nchini kwa lengo la kulitoa Taifa kwenye matumizi ya nishati zisiyofaa.


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la la Kitaifa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia amesema

Kikosi kazi hicho hakitakuwa cha Serikali pekee, bali kitahusisha pia sekta binafsi na wadau wa maendeleo na kitakuwa na kazi ya kuchambua sera za Serikali pamoja na mapendekezo ya wadau.


Alisema kikosi kazi hicho kitaongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa ngazi ya mawaziri na uratibu zote zitafanyika chini ya Wizara ya Nishati.


"Kikosi kazi hicho kitakuja na mpango mkakati ambao utaiongoza Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kutafuta suluhu ya nishati safi na endelevu ya kupikia" Alisema rais Samia.


Alisema kwa mujibu takwimu zilizopo kaya zinazopikia kwa kutumia mitungi ya gesi ni asilimia 5, umeme asilimia 3 na nishati nyingine safi asilimia 2.2.


Hivyo bado kuna kazi ya kubwa ya kuhamasisha matumizi ya nishati iliyo safi na salama na pia tunapaswa kuwa na mkakati madhubuti wa kisera na kibajeti pamoja na kuweka mazingira wezeshi katika kutatua changamoto za upatikanaji wa nishati safi.


“Serikali peke yetu hatuwezi tunapaswa kwenda sambamba na sekta binafsi, nashukuru baadhi yao wameanza kujitokeza kushirikiana nao sambamba lakini si kisera kutokana kuwa ni fursa ya biashara hivyo kuna haja ya kuwa na sera inayoshughulikia suala hili,” Alisema Rais Samia.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *