Torinto hot Media Blog.
Na Jerome Mlaki wa DAR
Mkurugenzi Tanzania Ajira Foundation, Allen Kimambo, akifafanua jambo wakati uzinduzi wa Programu ya Siku ya Waokota Taka Duniani ambayo kila mwaka uadhimishwa Novemba 2-9.
Afisa Tarafa Wilaya ya Ilala, Christina Kalekezi, akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Arch. Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija wakati wa uzinduzi wa Program ya Siku ya Waokota Taka Duniani inayoadhimishwa Novemba 2-9. Uzinduzi huo iulifanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 2, 2022.
Dar es Salaam - Tanzania: Kuelekea Siku ya Waokota Taka Duniani itakayoadhimishwa Machi 9, 2023, Taasisi ya TakaNiAjira na Nipe Fagio wameungana kuzindua 'Programu ya Siku ya Waokota Taka Duniani' ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuenzi na kuwatambua waokota taka na mchango wao katika sekta ya usimamizi wa taka nchini.
Mpango huu umeandaliwa ili kusherehekea Siku ya Waokota Taka Duniani katika namna muhimu kwa kuunda mfululizo wa matukio ambayo yataongeza usikivu na ufahamu kwa umma dhidi ya Wokota Taka, vyama vya ushirika katika sekta ya taka na wafanyakazi wa sekta hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mtengaji kutoka katika taasisi ya TakaNiAjira, Allen Kimambo alisema: “Tunafuraha kufanya kazi pamoja na Nipe Fagio katika kuzindua programu hii maalum ya kuwaenzi Waokota Taka na kutambua mchango wao katika sekta ya urejelezaji taka nchini Tanzania.”
Bw. Kimambo alisisitiza kuwa Siku ya Waokota Taka Duniani pia itasaidia katika kuziweka mbele changamoto zinazowakabili Waokota Taka na mahitaji yao na vyama vya ushirika vya taka nchini kote.
Alisema ingawa mchango wa Waokota Taka katika udhibiti wa taka ngumu ni muhimu, waokota taka wanakabiliwa na changamoto nyingi na vitisho katika maisha yao. "Waokota taka ni mojawapo ya makundi yaliyo hatarini ambayo yanakabiliwa na unyanyapaa na ukosefu wa usaidizi nchini" alisisitiza.
Alibainisha kuwa mpango huo utajumuisha usajili wa majaribio wa waokota taka kupitia Zaidi App na utafiti wa kutathmini hali ya sasa ya waokota taka na kubaini changamoto zinazowakabili.
“Tutafanya usajili wa majaribio na utafiti kuhusu hali ya sasa ya waokota taka na wafanyakazi katika mikoa 10 nchini ili kubaini changamoto zinazowakabili. Kupitia taarifa hizi tutakazozipata, tunaweza kusaidia vikundi hivi ipasavyo. Lengo letu ni kufikia angalau waokota taka 3,000 na wafanyakazi,” aliongeza. Mikoa hiyo 10 iliyochaguliwa ni Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza,Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Iringa, Ruvuma na Tabora.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Nipe Fagio akifafanua juu ya mfululizo wa matukio yatakayojumuishwa katika programu ya Siku ya Waokota Taka Duniani, Bi. Ana Le Rocha alisema: “Mbali na Mkutano wa Waokota Taka Duniani, ambayo ni siku ambayo tunasherehekea mafanikio yetu pamoja na Waokota Taka, vyama vya ushirika vya waokota taka, wafanyikazi, na wadau wakuu katika sekta ya usimamizi taka, kutakuwa na mfululizo wa matukio, ikiwa ni pamoja na Siku ya Huduma kwa Jamii ili kuwapa Waokota Taka huduma ambazo kwa kawaida hawawezi kuzipata.”
Mkutano wa Waokota Taka Ulimwenguni utawaleta pamoja waokota taka, wafanyakazi wasio rasmi, washikadau wa usimamizi wa taka, watoa huduma, vyombo vya habari, na umma katika sehemu moja ili kupeana stori za mafanikio, changamoto, matokeo ya tafiti na mfululizo wa jitihada mbali mbali ili kuhakikisha kutambuliwa kwa muda mrefu kwa watendaji hawa muhimu katika sekta ya usimamizi wa taka.
Baada ya Siku ya Waokota Taka Duniani, timu itaendesha kongamano la waokota taka mjini Dodoma ili kuwashirikisha wadau husika katika kujadili matokeo ya programu hadi kufikia hatua hiyo na nini kinapaswa kufanyika.
0 maoni:
Chapisha Maoni