WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 6 Juni 2017

 05:00      No comments


 TAGS
Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro  anatarajiwa kuzikwa kesho baada ya kufariki hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu,  kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo

Msemaji wa familia Shaaban Mtambo amesema kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo yamepangwa kufanyika siku ya Jumatano saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 

Alisema mke wa marehemu anatarajia kuingia leo mchana kutokea BanguiAfrikaKusini na watoto wake walioko Marekani ambao wanategemewa kuwasili leo usiku, kwaajiri ya mazishi.

Amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nyumbani kwa marehemu saa tano asubuhi siku hiyo ya Jumatano ambapo utafanyiwa kisomo na kuswaliwa kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.

 Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole kutwa nzima ya leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.


0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *