Torinto Hot Blog.
Na Joseph Maiko. Dar
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam, inayo ongozwa na Mstahiki Meya Isaya Mwita imepata hati safi kwa mara ya pili mfululizo.
Jiji la Dar es Salaam, limepata hati safi kutokana na ukusanyaji mzuri sambamba na kusimamia matumizi mazuri ya fedha.
Taarifa ya Mkaguzi na Mthibi mkuu wa hesabu za serikali [CAG] ya mwaka 2016 hadi 2017 iliyowasilishwa jana mbele ya baraza la madiwani ilieleza kuwa jiji hilo limepata hati safi kwa vipindi viwili mfululizo kutokana na usimamizi mzuri wa mapato.
Aidha Meya Mwita alisema kuwa kutokana na taarifa hiyo, imekuwa heshima kubwa na kuahidi kuzingatia maoni yalitolewa na ofisi ya CAG ili kuhakikisha kwamba jiji linaendeleza kupata hati safi.
Meya Mwita alisema kuwa hati hiyo iliyopatikana sio kwa juhudi zake pekee bali ni kutokana na ushirikiano mzuri anaoupata kutoka kwa Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana, Madiwani pamoja na watendaji wakuu wa halmashauri hiyo.
“ Mnapofanya kazi kama timu, kwa ushirikiano ndio inaleta mafaniko makubwa kama haya, nawashukuru madiwani wangu,tunafanya kazi vizuri ,wananipa ushirikiano mkubwa ndio mana tumefikia hapa tulipo” alisema Meya Mwita.
Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar e Salaam, Poul Makonda, Kaimu Mkuu wa mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva alimpongeza Meya Mwita na timu yake kwakusema kuwa wanakila sababu ya kupewa sifa kutokana na kazi kubwa wanayoifanya.
“ Kwaniaba ya Mkuu wa mkoa,niwapongeze kwa kupata hati safi kwa mara ya pili mfululizo,hii mnaonyesha ni namna gani mnafanya vizuri kwenye jiji lenu,lakini pia ninamna ambavyo mnasimamia na kutumia mapato yenu vizuri” alisema na kuongeza.
Wenzetu mnasimamia vizuri mapato yenu,Meya wangu wa Temeke hapa Abdallah Chaurembo ,kumbe moto ambao huwa unakuja nao kule ,unautoa huku,inabidi halmashauri nyingine muige mfano kutoka kwa meya wa Mwita ili mpeleke mafaniko kama haya kwenye halmashauri zenu” alieleza.
Mbali na pongezi hizo, Lyaniva alisema kuwa lipo suala la madeni ambapo wanasheria wa jiji wanapaswa kuhakikisha kwamba yanalipwa kwa wakati ili kuliongezea jiji mapato.
0 maoni:
Chapisha Maoni