WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 4 Juni 2018

 01:55      No comments


Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete (kushoto)  akipokea msaada wa futari kutoka kwa Arif  Yusuf wa Taasisi ya Dural Irshad Islamic Centre ya Dar es Salaam.

Aliyepo upande wa kushoto ni Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea misaada kutoka kwa Arif Yusuf. 

Sehemu ya misaada iliyotolewa.
toronto hot blog.
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete,  amepokea msaada wa futari kutoka kwa taasisi mbili za kidini, kwa ajili ya Waislamu waliopo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani jimboni humo.

Akipokea msaada wa futari hiyo iliyotolewa na taasisi za Dar Irushad Islamia Markaz na Miraj Islamic Centre za jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wananchi wasiojiweza, mbunge huyo amesema msaada huo utawafikia walengwa na kuzishukuru taasisi hizo kwa kuwakumbuka wananchi wanaoishi katika mazingira magumu katika mwezi wa Ramadhan.

Kwa upande, Arif Yusuf wa taasisi moja miongoni mwa zilizokabidhi misaada hiyo, ameeleza kwamba mwezi huu wa Ramadhan ni wa kumtegemea Mwenyezi Mungu na hivyo wameona ni vyema kula futari na wananchi wasiojiweza wa jimbo la Chalinze lakini akasema kwamba na wao misaada hiyo huipokea kutoka kwa taasisi mbalimbali za nje  ikielekezwa kuwaendea wasiojiweza.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *