Watu watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine takribani 7 kujeruhiwa vibaya baada ya Lori la mchanga aina ya SCANIA lililodaiwa kupata hitilafu katika mfumo wake wa breki kuwagonga.
Taarifa za ajali hiyo zinasema, ajali imetokea katika maeneo ya Boko Magengeni, jana Mei 7, 2018 ambapo inadaiwa lori hilo liliwaparamia watu waliokuwa pembezoni mwa barabara huku likisaga pikipiki kadhaa ambazo lilizipitia.
Kufuatia tukio hilo, RPC Kinondoni, Jumanne Murilo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema bado wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo hasa cha ajali hiyo.
Mbali na watu hao kupitiwa na roli hilo, zimo bodaboba na gari nyingine za abiria (coaster) ambazo zilipitiwa na lori hilo.
Pia inadaiwa wengine waliojeruhiwa ni wauza mitumba ambao hupanga kando ya barabara huku wengine wengi wakinusurika baada ya kukimbia walipoona ajali.
0 maoni:
Chapisha Maoni