Katibu Mkuu Tume ya utumishi wa walimu Tanzania Winfrida Rutahindurwa, amewataka walimu wakuu kusimamia taratibu na Sheria za kazi na kutoa muonekano haya Mwalimu yeyote atakaye enda kinyume cha Sheria bila kujali anauhusiano gani na kiongozi yeyote serikalini.
Ameyasema hayo wakati wa MKutano wake na walimu wa Maispaa ya Ilala uliofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee na kuwataka walimu wa nidhamu shuleni kuto wachapa viboko Wana funzi badala yake watumie mbinu nyingine walizo fundishwa ikiwemo adhabu ndogo ndogo.
"Wanafunzi wa kike wanapofikia umri wa kuvunja ungo wanabadilika wanapendeza nawaomba walimu wakiume wapendeni wanafunzi wa kike ila msiwatamani wapendeni kama watoto wenu mnavyo wapenda msiwape mimba msiwabake na kukatisha ndoto zao ukibainika adhabu ni kufukuzwa kazi hatanikikupa walimu wa kike msiwatamani wavulana " Amesema.
Kwa upande wa mavazi, amewataka walimu kuvaa nguo zenye staha na kuacha kuvaa nguo zenye picha mbaya na maandishi ya kutisha.
"Utakuta Mwalimu ameaahidi Nguza yenye picha ya chui katoa Meno mnawatisha wanafunzi, mimi nakumbuka nilipo kuwa na Soma Marangu tuliandamana kwa sababu Mwalimu wetu alikuwa anavaavibaya tuka goma kuingia darasani" Amesema.
Hatahivyo amewataka walimu kufundisha wanafunzi kwa bidii ili waweze kufaulu na kuwapa mazoezi ya mitihani ya kuwapima.
"Walimu wa Biology acheni kutumia vitabu vya Nyam bali Nyangwine ni bomu havifai kama kuna Mwalimu bado inatumia vitabu hivyo watafeli wote nilivangalia Sana nilipo kuwa wizara ya Elimu havifai" Amesema.
Amewataka pia kuacha kugoma na kuacha utoro na kuzingatia sheria za kazi huku akiagana kuwa mtumishi akidai Kisha siku tano hadi sita hajafika kazini kwa utoro anafukuzwa kazi na kuomba Kazi upya.
"Nataka ni waambie walimu kwa awamu hii ya tano kuomba kazi upya na kupata tena sirahisi ila Nawaomba walimu wakuu mazungumzo vizuri na walimu wasiingie kwenye makosa ya kinidhamu na wakiona rufaa wakashinda msiwatamani wepesi wa kuwa shitaki" Amesema.
0 maoni:
Chapisha Maoni