Mh. DC Sofia MJEMA AmePOKEA MSAADA KWA AJILI YA WATU WALIO ATHIRIKA NA MAFURIKO.
Torinto Hot Blog.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo amepokea Msada wa vyakula na bidhaa mbalimbali kutoka kwa Jumuiya Khoja Shia Ishanashari Kamat na IST kwaajili ya wana nchi na shule za umma zilizoathirika na Mafuriko katika wilaya ya Ilala.
Akizungumza wakati anapokea msaada huo Mh. Mjema amesema katika wilaya hiyo jumla ya nyumba 70 na shule moja zote ziliathirika na mvua katika kipindi cha mwezi April na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam, na kwamba Kuna watu Misaada hiyo itawasaidia kwa kuwa vitu vyao vingi viliharibiwa na Maji.
"Tuna shukrani Sana ndugu zetu hawa wamekusanyana wamechanga jumla ya shilingi milioni kumi wamenunua hivi vifaa, wametuletea Masink ya vyoo mia moja, water guard, biscuits, Freestyle kwaajili ya akina mama, Taulo, vitabu, madaktari takribani vifaa hivi ni vya watu mitano. "Amesema Mjema.
"Misaada hii itapelekwa kwa familia zilizopata mafuriko zote kila mtu itamfikia"alisema Mjema.
Kwa upande wao waliotoamsaada huo akizungumza mara baada kukabidhi msaada huo Dewji amesema, shule yao ya Tanganyika inafundisha watoto wa miaka minne hadi 12,mara baada kutokea mafuriko hayo wanafunzi wa shule hiyo waliguswa.
"Wanafunzi wa shule yetu wameguswa wameungana na Serikali leo tumekabidhi msaada wetu kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema "alisema Dewji.
0 maoni:
Chapisha Maoni