MKURUGENZI GENZI KIGAMBONI KUWEKWA KITI MOTO KWA KUPU UZA AGIZO LA SERIKALI.
Na. Jerome Mlaki.
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lianiva amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya kigamboni kuanzisha baraza la wafanyakazi pamoja na kuandika barua ya kujieleza kwa nini hajaanzisha baraza hilo.
Kauli hiyo ameitoa Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambapo alipokua akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, alisema baruua hiyo inatakiwa iwasilishwe ofisini kwa Mkuu wa mkoa mapema.
Baadhi ya vyema vya wafanyakazi vilivyoshiriki katika madhimisho hayo ambapo vilikua vimebeba ujumbe mbalimbali ni Banki ya CRDB, Kituo cha utangazaji wa habari TBC, Chama cha walimu pamoja na mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF.
Aidha alisema,Serikali ya awamau ya tano ni sikivu na makini sana hivyo itahakikisha inatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kuwaondolea kodi katika mshahara na mabaoni pamoja na kuboresha kuleta mahusiano mazuri kazini.
Kwa upande wake, Katibu wa Tuico Kanda ya Dar es Salaam, Innocent Alute amesema Chama cha wafanyakazi kinakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kukatwa kodi kubwa katika mishahara,baadhi ya waajiri kukwepa sheria ya ajira na mahusiano kazini ya 2006.
Amesema kuwa, baadhi ya Manispaa hazina baraza la wafanyakazi ikiwemo manispaa ya kigamboni tangu ilipoanzishwa baraza hilo, jambo ambalo linrudisha nyuma harakati za maendeleo kutokana na kuwa baraza hilo ndio chombo pekee cha kuweza kutoa maoni na kufanyiwa kazi.
Ameongeza kuwa, mikopo Bodi ya mikopo iangalie upya utaratibu waliouchukua wa kukataa asilimia 15 kwa wafanyakazi badala ya asilimia 8 walivokubaliana kwenye mkataba kwani kuendelea kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
0 maoni:
Chapisha Maoni