Mwenyekiti wa Mtaa wa Msigwa aelezea mafanikio katika uongozi wake
Na Torinto HOt Blog.
MWENYEKITI wa Mtaa Msigwa kata ya Bonyokwa Hassan Ngimbi amefanikiwa kujenga barabara Mpya 18 katika kipindi cha uongozi wake kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa .
Mwenyekiti Hassan alisema Mtaa wake una wakazi 3000 kaya 633 kwa sasa
Kisima kimoja cha MAJI salama kinahudumia wakazi wa Mtaa huo kinauwezo wa kuzalisha Lita 20000 .
" Katika uongozi Wangu nimefanikiwa kuboresha miundo mbinu yote katika Mtaa huu japo changamoto ya Jiografia ya milima lakini kwa ushirikiano wa MANISPAA Yangu na utekelezaji wa Ilani nimeweza kufufua barabara 18 awali zilikuwa 14 kwaiyo kwa sasa mtaa Wangu una barabara 32 zinapitika" alisema Hassan..
Alielezea mafanikio mengine ameweza kuongeza madarasa mawili katika Shule ya msingi Kifuru Na matundu ya vyoo .
Mafanikio mengine ujenzi wa OFISI ya Mtaa ujenzi unaendelea upo katika hatua ya linta.
Kuhusu changamoto Mtaa huo amna zahanati na Shule ya Sekondari changamoto nyingine wananchi wake ndoo ya MAJI wananua kwa sh.500 hadi 1000 na miundombinu nyakati ya mvua shida.
Aidha aliwataka wananchi wa Mtaa huo kushirikiana katika kuleta Maendeleo ya Mtaa wao na kuibua miradi itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi .
0 maoni:
Chapisha Maoni