WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 24 Januari 2018

 02:52      No comments

Madiwani jiji la Dar es salaam walalamikia mapato ndani ya soko la kariakoo.


NaTorinto Hot Blog.

Baraza la madiwani Dar es salaam limefanya kikao ambacho ni kikao cha  kawaida cha robo ya mwaka ambacho  kimeongozwa  na mwenyekiti wa baraza hilo Isaya Mwita ambapo zimejadiliwa ajenda mbalimbali zinazohusu maendeleo ndani ya jiji la Dar es salaam.

Moja ya hoja iliyowasilishwa ni kuhusu mapato yanayopatikana ndani ya soko la kariakoo ambapo imeonekana kuwa soko hilo limekuwa likisababisha hasara kubwa sana ndani ya mapato ya jiji la Dar es salaam.

Akichangia hoja hiyo diwani kutoka kinondoni Abdallah Mtinika amesema kuwa soko hilo limekuwa na changamoto nyingi kwa Kipindi kirefu lakini hakuna ufumbuzi wowote uliopatikana na kuomba mwenyekiti wa Baraza kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo.

"Soko la kariakoo limekuwa likisababisha hasara kubwa kila mwaka na hakuna ufumbuzi uliopatikana hivyo tunaomba mwenyekiti utolee ufafanuzi jambo hilo" amesema Mtinika.

Kwa upande wake mwenyekiti akijibu hoja hiyo amesema kuwa suala hilo wameshaliongelea na imebainika kuwa ni kweli soko hilo limekuwa likisababisha hasara kubwa sana na kuongeza kuwa wameshaongea na uongozi wa kariakoo na umeahidi kufanya maboresho na mabadiliko ndani ya soko hilo.

Pia mwenyekiti amesema kuwa wameamua kuwapa muda wakuu wa masoko la kariakoo ili waone utendaji wao kwani uongozi huo umeahidi kuja na mabadiliko makubwa kwa mwaka huu sambamba na kuonyesha ripoti ya mapato yanayopatikana ndani ya soko.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *