KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI (TAA) ATEMBELEA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye kushoto akimkaribisha Kaimu Mkuu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela kulia alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 23/01/2018.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ziara yake mapema leo tarehe 23/01/2018.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (aliyeketi mbele) pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo wakimfuatilia kwa karibu, Kaimu Mkurugenzi MKuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, wakati wa mazungumzo yao alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 23/01/2018.
Picha ya Pamoja, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa pili kushoto) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela (wa tatu kulia), mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 23/01/2018.(Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
0 maoni:
Chapisha Maoni