WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 24 Januari 2018

 02:57      No comments

“NABII” TITO ATIWA MBARONI MJINI DODOMA LEO


1
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akimsikiliza mhubiri wa kujitegemea ajiitaye Nabii Tito ambaye ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kutoa maneno yaliyo kinyume na maadili. Nabii Tito anashikiliwa nan a jeshi hilo kituo cha kati mjini Dodoma. Taarifa kamili itafuata baadaye.
2
Nabii Tito akiwa chini ya ulinzi Central Police Dodoma leo. 
……………………
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Marlin Komba amesema hamtambui mtu anayejiita nabii Tito na kwamba hajasajili kanisa lake katika ofisi ya msajili wa taasisi za dini, na kwamba Serikali imeona vitendo anavyovifanya ‘nabii’ huyo kupitia mitandao ya kijamii na imeanza kuchukua hatua.
“Ninachoweza kusema ni kwamba hakuna mtu anayezuiwa kuongea hapa nchini, mwache aongee anavyoweza ila Serikali imeshaona anachokifanya na yanayoendelea mitandaoni hatua zinachukuliwa dhidi yake,” amesema Komba.
Kauli hii imekuja kufuatia kusambaa kwa video mbalimbali zikimuonyesha ‘nabii’ huyo akitoa mafundisho yake huku akinywa vilevi pamoja na kufanya matendo ambayo ni kinyume cha maadili ya dini, jambo ambalo limeonekana kuwakera wadau wengi wa dini.
Kwa upande wao viongozi mbalimbali wa dini wameonyeshwa kukerwa na kulaani vitendo anavyovifanya mtu huyo anayejiita ‘nabii’ na kusisitiza kuwa hakuna dini inayoruhusu hayo.Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza amesema kuwa, kutokana na vitendo anavyofanya, mtu huyo hapaswi kujiita mtumishi wa Mungu.“Huyo hawezi kuwa mtumishi wa Mungu na wala hafanyi huduma ya kanisa. Ni vyema watu kama hawa wafuatiliwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
 "Natumaini Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndani yake ina ofisi ya msajili wa taasisi za dini itafanya kazi yake,” amesema Mchungaji Lwiza.
Naye Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Rajab Katimba amesisitiza Serikali na viongozi wa dini kuingilia kati suala hilo na kueleza kuwa, hakuna kitabu chochote cha dini kinachohamasisha ulevi na ukosefu wa maadili.“Hilo suala linakwenda tofauti na dini na mila na desturi zetu pia. Dini zinatakiwa kuleta amani na kuhamasisha watu waheshimiane si kuzungumza mambo yanayokiuka maadili yetu. 
"Naona ipo haja ya viongozi wa dini na Serikali kuingilia suala hili na waende mbali zaidi kwa kuongea naye huenda hafahamu anachokifanya,” amesema Rajab Katimba.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *