RC Makonda akifanya zoezi LA ujenzi baada ya uzinduzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amezindua zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema ujenzi wa Ofisi hizo utaenda kwa kasi ya hali ya juu chini ya Vijana wenye morali ya kazi kutoka JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.
Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Walimu wa kawaida, Mhasibu, Karani, Chumba cha kuhifadhi Mitihani, Vyoo vya kisasa, Stoo, Jiko, Chumba cha Mikutano na sehemu kuweka Mafaili ambapo ndani ya ofisi zitafungwa AC, Feni, Samani, Taa za kisasa na Umeme.
Akizungumza Katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na upandaji wa Miti *RC MAKONDA* amesema kuwa *lengo la ujenzi huo ni kuwezesha Walimu kufanyakazi katika Mazingira mazuri* yatakayowapa morali na hamasa ya kufundisha Wanafunzi.
Aidha MAKONDA amesema kama Walimu wakiboreshewa Mazingira ya kufanya kazi itasaidia kukuza ufaulu.
MAKONDA amepongeza Walimu kwa kuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa Darasa la saba ikitokea nafasi ya nne mwaka jana na kuwahimiza kukamatia nafasi hiyohiyo.
"Rais MAGUFULI ameshatuonyesha dira kwa kutoa elimu bure na sisi wasaidizi wake ni lazima tuendeleze maono yake, mimi sio kiongozi wa kusubiri kuagizwa ndio nifanye kazi kama ilivyo kwa Remote hadi ibonyezwe ndio ifanye kazi, mimi ni kiongozi wa kujiongeza, sijachaguliwa kuwa mzigo kwa serikali bali kuleta matumaini kwa wananchi"Alisema.
Amewataka Viongozi kuacha Siasa kwenye mambo ya Msingi yanayolenga kuleta maendeleo kwakuwa Maendeleo hayana chama wala ubaguzi wa Dini.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Kamanda wa Polisi kanda maalumu Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule ambapo Wote kwa pamoja wamepongeza hatua ya MAKONDA kujenga ofisi za Walimu.
0 maoni:
Chapisha Maoni