Na Joseph Lieme, Torinto Hot Blog.
Madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kutii Sheria za barabarani na kuepuka uzembe,ili kutokomeza na kupunguza ajali za Mara kwa Mara zinazosababisha vifo kwa watanzania kwani atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Hayo yamesemwa Leo nakamanda wa kikosi cha usalama barabarani Fortinatus Muslim wakati akizungumza na waandishi WA habari ambapo amewataka madereva kuepuka uzembe na kutii Sheria bila shuruti kwani atakaye sabababisha ajali kwa kutofuata Sharia sa usalama barabarani hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
"Ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani, mkoa wa Dar es Salaam Tunatarajia kuadhimisha ifikapo tarehe 18 hadi 25 November mwaka huu, kinondoni kwenye viwanja vya Biafra Lengo letu likiwa ni kuangamiza kutokomeza kabisa ajali sa barabarani."Amesema.
Aidha amesema katika kusisitiza na Kutoa elimu mbalimbali kwa madereva juu ya usalama barabarani pamoja na kuzingatia Sheria za barabarani kumeanza kuzaa matunda hadi kufukia Sasa, kwani kumepnguza ajali za Mara kwa Mara.
Kwa upande wake Musa kitoi ambaye ni Mkuu wa tawi la Stan bank ambao ni wadhamini wa maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika November MW aka huu, amesema kuwa wamewezakutambua umuhimu wa kutoa elimu kwa jamii juu ya kukabiliana na ajali za barabarani, hii itasaidia kupunguza ajali za barabarani na ndio maana wameamua kushirikiana na jeshi la polisi ili kuokoa maisha ya watanzania wanaofariki kutokana na ajali.
"Tumeguswa na tumeamua kuchangia ili kusaidia kupaza sauti za jeshi la polisi katika zoezi hili waweze kuwafikia watu wengi na waweze kupata uelewa zaidi juu ya suala la kutokomeza kabisa ajali za barabarani" Amesema kitoi.
Aidha ameeleza mikakati ya Stan bank katika kutoa elimu kwa jamii kiurahisi na kusema kuwa wameweza kuandaa video, stika zenye ujumbe utakao toa elimu kiurahisi na watu maalum watakaosaidia kutoa elimu hasa kwa madereva wanaobeba wanafunzi.
Pia ameziasa taasisi nyingine za kifedha kuunga mkono jeshi la polisi kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu hivyo wakiungana kwa pamoja wataweza kutokomeza kabisa vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.
0 maoni:
Chapisha Maoni