Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Isack Sawala, alisema tukio hilo likitokea juzi baada ya mvua kubwa kunyesha ikiambatana na upepo mkali.
Hata hivyo, alisema hakuna mtu aliyefariki dunia kutokana na tukio hilo, lakini baadhi ya watu walijeruhiwa na kupelekwa katika Kituo cha Afya cha Matai kwa matibabu.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo, Frank Sichalwe, alisema nyumba nane zimebomoka kabisa na hazifai kuishi tena binadamu na wananchi hao wanahitaji msaada wa hali na mali.
Alisema kamati ya maafa ya wilaya inaendelea na jitihada za kuwasaidia wananchi hao ambao wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na tukio hilo.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi wenye mapenzi mema kutoa misaada ya kibinadamu, ili kuwasaidia wananchi hao kwa kuwa wanahitaji hifadhi kwa ajili yao na mali zao kwa kuwa hawana makazi ya kuishi.
Katika hatua nyingine, alitoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanajenga nyumba kwa kutumia saruji tofauti na sasa kwa kuwa baadhi ya wananchi wamejenga kwa kutumia udongo hali inayosababisha nyumba hizo kutokuwa imara.
0 maoni:
Chapisha Maoni