WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 11 Oktoba 2017

 05:14      No comments


 TAGS
Fuvu la kichwa lililokutwa kwenye bwawa la maji.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule amethibitisha kuokotwa kwa viungo vya mwili wa binadamu katika bwawa la maji la Jomu wakati watu wakitafuta maji huko Tinde mkoani Shinyanga.

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule amedai kuwa jana watu walipoona viungo hivyo vya binadamu ilibidi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na wao walifika na kukuta viungo hivyo.

"Fuvu la kichwa limepatikana hapo bwawani, taya ya binadamu, mbavu za binadamu kumi na nne, baada ya kupatikana kwa taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka kufika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa awali tukishirikiana na daktari mtaalam wa viungo vya binadamu katika tukio hilo tulikuta viungo hivyo ikiwa pamoja na mfupa mmoja wa sehemu ya paja, mifupa ya mikono na mifupa ya sehemu ya bega ya binadamu" alisema Simon Haule

Aidha Kamanda Haule amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ikiwa pamoja na kufungasha mifupa yote na kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanya vipimo kubaini vinasaba na jinsia ya mtu ambaye amefariki.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *