mkurugenzi mkuu wa makampuni yote yanayounda jina la HANSPAUL bwn.Satbir Singh Hanspaul kutoka jijini Arusha akizungumza na waandishi wa Habari alipofika jijini Dar es salaam kushiriki mkutano wa mwaka wa jumuiya ya serikali za mitaa tanzania (ALAT)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3CN_fiAoOJO5k_bhesO2v4lc6a32SeVt-UCTtwkkrz1OMBiJn_bAwKw4lFWEFDnoW_nxm_nHb09U7YC3VMy6iROia1YJZ5D0kKvFwtqHGIHRXkeAKSOI65ILsBOe1K6OQtBegS_kuNGk/s640/IMG_20171002_171846+%25281%2529.jpg)
Moja ya gari maalumu la kubebea taka gari ambalo ni maalumu na zuri katika shuhuli za kiusafi katika miji pamoja na mitaa mbalimbali ambalo huzalishwa na kampuni hiyo ya HANSPAUL
Na mwandishi wetu Joseph Lieme Dar.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya HANSPAUL Bwn.Satbir Singh Hanspaul ambao ni wazalizashaji wa vifaa vya magari maalumu kwa ajili ya kuzolea taka taka pamoja na magari aina ya matrekta kutoka Mkoa wa Arusha ameonyesha kufurahishwa na kasi ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.John pombe Magufuli kwa kusema kuwa kitendo cha Raisi kupenda maendeleo ya wananchi wake limekuwa ni jambo jema kwake na pia linaonyesha ni njia ya kipekee katika kuwaokoa wengi wa wa tanzania katika sekta nzima ya viwanda na Biashara.
Awali akizungumza pamoja na chombo hiki kilipofika katika moja ya banda maalumu lenye maonyesho ya bidhaa ambazo kampuni yake inazalisha Bwn. Hanspaul ameonyesha zaidi kufurahishwa na juhudi za Rais hasa kwa kitendo cha rais Magufuli kuamua kuhamishia mkutano huo wa mwaka ambao ulikuwa ufanyike kitaifa katika mkoa wa Mbeya lakini kutokana na rais kutamani kukutana na baadhi ya wahusika katika utendaji wa serikali katika ngazi ya mtaa pamoja na Wadhamini husika wanaounga mkono juhudi za Kasi ya maendeleo hapa nchini na kutokana na rais kuwa na shuhuli nyingi wao wamefurahishwa na kitendo hicho cha kuamua kuhamishia mkutano huo kuanyika Dar es salaam badala ya Mkoa wa Mbeya
Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika mapema siku ya kesho 03.10.2017 huku mgeni rasmi akiwa ni Rais Magufuli wapo wawekezaji wengi ambao wamejitokeza kuunga mkono mkutano huo ikiwa ni pamoja na Kampuni hii ya HANSPAUL kampuni hii wamefika Dar es salaam ikiwa ni moja ya njia katika kuitangaza bidhaa zao katika masoko na kupatikana kwao ni ukifika tuu katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Mwl Nyerere kwenye banda lao la maonyesho kabla tuu ya kuingia ndani ya mkutano
Hivyo katika kutoa wito kwa watanzania pamoja na kuunga mkono juhudi za kuuunga mkono bidaaa ambazo huzalishwa hapa nchini kutoka kwenye kampuni hizo za HANSPAUL kutoka Arusha Njiro
Kampuni hii ya HANSPAUL ni muunganiko wa kampuni kubwa ambazo zote kwa pamoja zinazalisha bidfaa mbali mbali na majina ya kampuni husika ni pamoja na HANSPAUL AUTOMECHS LTD,HANSPAUL INDUSTRIES LTD,DHARAM SIGNH HANSPAUL&SONS LTD
0 maoni:
Chapisha Maoni