WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 13 Septemba 2017

 04:06      No comments


YAMAPITIO

SERA YA TAIFAUTALII YA MWAKA 1999
TAREHE 13/09/2017 MKOANI DAR ES SALAAM

Seraya Taifa ya Utalii iliandaliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1991 na
kuhuishwa mwaka 1999 kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii
yaliyotokea hapa nchini, hususan Serikali kujiondoa katika umiliki na
uendeshaji wa biashara ya huduma za kitalii na kuiachia sekta
binafsi.Tangu kuhuishwa Sera hii imechukua takriban miaka 17 ambapo
kuna mabadiliko makubwa yaliyojitokeza katika kipindi hicho hususan
mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kimazingira na teknolojia. Kutokana na
msukumo wa mabadiliko hayo na ukuaji wa sekta hii inatulazimu kufanyia
mapitio Sera hii ili iendane na mabadiliko hayo.

Kazi hii inafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia ofisi ya Waziri Mkuu na
Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT). Aidha, Mtaalamu Mwelekezi
wa hiii ni Economicand Social Research Foundation(ESRF). Kazi hii
imepangwa kufanyika kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza ilikuwa
ni kuandaliwa kwa inception report na kuwasilishwa Wizarani, awamu ya
pili ni kukusanya maoni ya wadau wa utalii kwa ajili ya mapitio ya Sera
zoezi ambalo tumeshafanya katika Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa,
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati na
leotunafanya Kanda ya Pwanihapa MkoaniDar es Salaam na baadae
kuendelea na kanda zilizosaliaambazo ni; Kanda ya Kusini na Warsha
moja itafanyika Zanzibar. Lengo ni kupata maoni ya wadau ili yajumuishwe
kwenye Sera Mpya inayoandaliwa ili kufanya sekta hii iendelee kukua na

2 | Page
kukuza uchumi wa taifa. Baada ya warsha hizo Wataalamu watafanya
ulinganifu wa Sera yetu na sera za nchi nyingine ambazo zinaendesha
utalii unaofanana na utalii wa Tanzania kwa lengo la kujifunza na
kuboresha zaidi Sera yetu.

Baada ya awamu hii itaandaliwa rasimu ya kwanza ya Sera ya Taifa ya
Utalii. Awamu ya tatu itakuwa ni kufanya mkutano wa kamati ya kitaifa ya
kupitia Sera(National Consultative meeting/validation process)na
kuwasilisha rasimu ya kwanza kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi Maliasili na Utalii na awamu ya mwisho itakuwa ni kuandaarasimu
ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Utalii itakayowasilishwa Serikalini na
baadaye kusambazwa kwa wadau kwa ajili ya utekelezaji.

Ndugu Washiriki
Napenda kutumia fursa hii kuwakaribisha wote katika mkutano huu muhimu
ili kutoa michango yenu itakayosaidia kukamilisha Sera Mpya na hivyo
kuwa na sekta ya utalii yenye dira makini kwa ukuaji na ustawi wa utalii
nchini.

Baada ya kusema hayo machache,kwa heshima kubwa namkaribisha
Mwenyeji wetu, RAS Mkoa wa Dar es Salaam ilikutoa salamu zake.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *