WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 13 Septemba 2017

 04:05      No comments


TAREHE 13 SEPTEMBA, 2017


Ndugu,
Katibu Tawala Mkoa wa Dar Es salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Utalii,
Mtaalamu Mwelekezi,
Wawakilishi wa Asasi mbalimbali za Sekta ya Utalii Kanda ya Pwani,
Wageni waalikwa,
Mabibi na Mabwana,

Ninayo furaha kubwa kujumuika pamoja nanyi leo katika warsha hii muhimu ya
kuendeleza mchakato wa kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999.
Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wote mtakaoshiriki warsha hii
iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kukusanya maoni yatakayojumuishwa katika
Sera mpya ya Taifa ya Utalii. Ni matumaini yangu kuwa mtashiriki kikamilifu
kutoa maoni yenu ili tuweze kuwa na dira nzuri ya sekta hii yenye mchango
mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa letu. Ninatambua kuwa, warsha hii
imeshirikisha wadau wa utalii kutoka mikoa miwili ya Kanda ya Pwani ambayo ni;
Dar es Salaam na Pwani.

Ndugu Washiriki,
Nichukue fursa hii kipekee, kuwashukuru wadau wetu wakubwa wa maendeleo
Benki ya Dunia (WB) chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kutoa
ushirikiano wa kuwezesha warsha hii katika kanda mbalimbali ikiwemo kanda ya
Pwani ambayo inafanyika leo hapa Mkoani Dar es Salaam. Aidha, nawashukuru
pia wadau wa Sekta Binafsi Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT) kwa
kuwezesha warsha kama hii kufanyika. Ushirikiano wa namna hii ndio

2
utawezesha kuendeleza sekta ya Utalii na Ukarimu kwa kiwango cha juu na
hivyo kukuza uchumi wa taifa letu.

Ndugu Washiriki,
Ikumbukwe kuwa, Sera ya Taifa ya Utalii iliyopo ilifanyiwa mapitio kwa mara ya
mwisho mwaka 1999 ambapo ni takribani miaka 17 iliyopita. Katika kutambua
hilo, Wizara imeanza kupitia upya Sera hii ili kuhakikisha Sekta ya Utalii inakidhi
changamoto zinazotokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea duniani
yakiwamo ya teknolojia, kijamii, kiuchumi, kisiasa na mazingira.

Aidha, misingi ya kuandaa Sera yeyote ni pamoja na kushirikisha wadau wote
muhimu ambao ndio watekelezaji wa Sera hiyo. Tukizingatia ya kuwa Sekta ya
Utalii inaendeshwa kwa kiasi kikubwa na Sekta Binafsi katika kutoa huduma na
kufanya biashara za utalii hapa nchini, tunategemea kupata maoni na michango
yenye tija itakayowezesha upatikanaji wa Sera bora itakayoleta ufanisi katika
uendeshaji wa huduma zinazotolewa katika sekta hii. Kwa kutambua mchango
wa utalii kwa maendeleo endelevu ya taifa letu, ni wazi kuwa tunahitaji Sera
wezeshi yenye kutoa mwongozo wa utaratibu bora na sahihi wa usimamizi,
uendelezaji na utendaji katika sekta ya utalii nchini.

Ndugu washiriki,
Wote tunaelewa ya kuwa sekta ya Utalii ni moja wapo ya sekta zinazokua kwa
kasi na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi. Takwimu
zilizopo zinaonyesha kuwa, sekta ya utalii inachangia 17.5% ya Pato la Taifa
(GDP) na huliingizia Taifa fedha za kigeni (asilimia 25).

Ukuaji wa sekta hii, umedhihirika pale ambapo katika miaka ya hivi karibuni
mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka Dola za Kimarekani bilioni 1.7
mwaka 2012 hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2.1 mwaka 2016. Ongezeko
la mapato hayo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka
1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,284,279 mwaka 2016.

3
Ukuaji huu wa sekta ya utalii umechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi za
Serikali katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali, utangazaji
katika masoko mbalimbali duniani utalii, mazingira bora ya uwekezaji pamoja na
ushirikiano madhubuti baina ya sekta za umma na binafsi kwa kuzingatia kanuni
na taratibu zilizopo. Hata hivyo ukuaji huu hauwiani na rasilimali nyingi tulizonazo
ambazo ni nzuri, na za kuvutia ukilinganisha na nchi jirani ambao ni washindani.
Tunapaswa sasa tukae pamoja tujadili na kutoa michango yetu ya dhati
itakayotuwezesha kupata dira ya kutuongoza katika kuinua mchango wa sekta hii
na hivyo kukuza uchumi wa nchi yetu.

Ndugu washiriki,
Tuna kazi kubwa iliyoko mbele yetu, ni vyema sasa kuweka mawazo yetu kwa
pamoja katika kipindi cha masaa machache yajayo na kuibuka na maoni mazuri
yatakayojumuishwa kwenye Sera mpya ya Taifa ya Utalii.

Baada ya kusema haya machache, ninayo furaha kutamka kuwa Warsha hii ya
kukusanya maoni ya wadau wa kanda ya Pwani kwa ajili ya kupitia upya Sera ya
Taifa ya Utalii ya mwaka 1999, imefunguliwa rasmi.

AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA NA NAWATAKIA MAJADILIANO
MEMA

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *