Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 utawasili kesho Tarehe 31 Mei 2017 katika Wilaya ya Ubungo kuanzia saa moja kamili asubuhi na kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Mradi mmoja wa kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la msingi.
Alisema kuwa Miradi mingine itakayozinduliwa ni Mradi wa Ujenzi wa Jengo la kutolea huduma za VVU katika Kituo cha afya Mbezi, Uzinduzi wa madarasa nane katika shule ya Msingi Malambamawili iliyopo Kata ya Msigani, Uzinduzi wa Kituo cha mabasi SIMU 2000 Kata ya Sinza na Uzinduzi wa Zahaanti ya Mburahati.
Mhe Makori alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu Bilioni 2,854,647,991.89
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amewasihi wakazi wa Manispaa ya Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru ambao utawasili katika eneo la SAISAI Kata ya Gobaukitokea Manispaa ya Kinondoni.
Pia amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Barafu, Shule ya Msingi Mburahati kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru.
0 maoni:
Chapisha Maoni