Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzabia Dkt. John Magufuli, amemteua kamishina wa polisi Simon Sirro kuwa mkuu wa jeshi la polisi (IGP).
Kabla ya uteuzi huo IGP Simon Siro alikuwa kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam.
IGP Simon Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.
- Magufuli amfuta kazi waziri wa nishati
- Lowassa: Kuna dalili za 'udikteta' serikalini Tanzania
- Nnauye: Bado naunga mkono juhudi za Magufuli
Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu kiongozi balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa kesho Jumatatu katika Ikulu ya jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni