Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kutoka hisa Milioni 7 hadi hisa 745,000 ingawa Mauzo ya hisa yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 4 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 6 wiki hii.Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:TBL …………………………………………..……..98.1%SWISSPORT …….………………..…………..………0.82%CRDB ……………..……….…………....……………0.60%Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umeongezeka kwa Shilingi Trilioni 1 kutoka Shilingi Trilioni 19.3 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 20.2 wiki iliyoishia tarehe 5 Mei 2017. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za JHL (20.3%), ACACIA (13.8%) na EABL (2.9%).Mtaji wa kampuni za ndani pia umeongezeka kwa Shilingi Bilioni 48 kutoka Shilingi Trilioni 7.303 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.351 wiki hii. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za TBL (1.8%).Viashiria (Indices)Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimeongezeka kwa pointi 106 kutoka pointi 2,221 hadi pointi 2,327 kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.Kiashiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimeongezeka kwa pointi 22 kutoka pointi 3,475 wiki iliyopita hadi pointi 3,497 wiki hii.Sekta ya viwanda (IA) imeongezeka kwa pointi 52 kutoka pointi 4,437 wiki iliyopita hadi pointi 4,489 wiki hii kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za TBL kwa asilimia 1.8%.Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepungua kwa pointi 3 kutoka pointi 2,546 hadi pointi 2,543 kutokana na kupungua kwa bei ya hisa za DSE kwa asilimia 8%.Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imepungua kwa pointi 105 kutoka pointi 3,137 hadi pointi 3,032 kutokana na kupungua kwa bei ya hisa za SWISSPORT (4.6%).Hati Fungani (Bonds)Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 5 May 2017 yameongezeka kutoka thamani ya Shilingi Bilioni 4.5 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 27.1.Hii ilitokana na mauzo ya hati fungani kumi na tatu (13) za serikali na hati fungani moja ya EXIM zenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 36.6 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 27.1.Shindano la Wanafunzi la UwekezajiUSAJILI katika Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 bado unaendelea. Hadi sasa vyuo vitatu (3) vinavyoongoza katika idadi ya wanafunzi wanaoshiriki ni:CHUO CHA MIPANGO (IRDP) …………………………………………..…….. 342CHUO CHA UHASIBU ARUSHA (IAA) ……………..……….…………....….. 341SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE (SUA)…………………….……… 217Na vyuo tano (5) vinavyoongoza kwa washiriki wachache hadi sasa ni:UNIVERSITY OF DODOMA …………………………………………………………….. 83UNIVERSITY OF IRINGA …………………………...……………………………………. 13ZANZIBAR UNIVERSITY ……………………………………………………..……... 3MOUNT MERU UNIVERSITY……………..……….…………....………………….…. 1 BUTIMBA TEACHERS COLLEGE ………..…………………………………………….. 1Vile vile Shule za Sekondari zinazoongoza kwa idadi ya wanafunzi wanaoshiriki ni:LOYOLA HIGH SCHOOL ……………..……….…………... 35DAR ES SALAAM INDEPENDENT SCHOOL (DIS) ……. 22SHAABAN ROBERT SECONDARY SCHOOL ……………….. 17Na Shule tano (5) za Sekondari zinazoongoza kwa washiriki wachache ni:Jangwani Girls Secondary School …………………………… 2Minaki High School ………………………………………………… 2Kitumba Secondary School …………………………………….. 1International School of Tanganyika ……………………….. 1Arusha Secondary School ………………………………………. 1
Kind regardsPatrick Mususa
Jumatatu, 15 Mei 2017
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni