TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Benki ya EXIM yapata faida ya bilioni 83.6
Aprili 3 2017, Dar es Salaam
Benki ya Exim imepata faida ya Tsh bilioni 83.6 (kabla ya kodi) kwa mwaka wa fedha 2016 ikiwa
imejumuisha faida ya Tsh bilioni 46.4 ya kuuza hisa ilizowekeza. Faida itokanayo na uendeshaji wa
shughuli mbalimbali za kibenki ni Tsh 37.2 Bilioni.
Mapato yatakanayo na riba yaliongezeka kwa asilimia 25 mpaka Tsh 90.9 bilioni, ikiwa imechangiwa na
ongezeko la mikopo pamoja na mkazo katika amana zenye riba nafuu.
Aidha katika kipindi hicho hicho, mapato yatokanayo na tozo mbalimbali za huduma za kibenki
yaliongezeka kwa asilimia 14 mpaka Tsh bilioni 35.7 ukilinganisha na Tsh bilioni 31.3 kwa mwaka
uliopita. Ukuaji huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ufanisi kwenye utoaji huduma kwa wateja
wakubwa na wale wa kati.
Faida hiyo imeongeza mtaji wa benki kufika Tsh bilioni 227 na kuongeza uwezo wa benki kuweza
kufanya miamala ya kibiashara mikubwa zaidi.
Katika kuongeza uwezo wa kutoa huduma nzuri kwa wateja na kujiandaa kwa ukuaji wa kasi, Benki ya
Exim ametelekeza miradi mbalimbali ya kiteknolojia. “Nina furaha kubwa kuwataarifu kwamba kati ya
miradi 8 ya kiteknolojia, miradi 7 imemalizika kwa mafanikio”. Alisema Afisa Mkuu wa fedha wa benki
hiyo Bw. Selemani Ponda na kusisitiza kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia, benki itaweza kutoa
huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Utekelezaji wa miradi hiyo kwaajili ya kubadilisha mifumo ya kiutendaji umepelekea uwekezaji mkubwa
katika rasilimali watu na teknolojia na hivyo kusababisha gharama za uendeshaji kupanda. Katika taarifa
yake ya fedha jumla ya gharama ya uendeshaji ilipanda kwa asilimia 24 hadi kufikia Tsh bilioni 99.
Benki ya Exim imejiandaa kuwahudumia wateja wa kada zote kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa
kuhudumia wateja wote mara baada ya kutekeleza miradi ya kiteknolojia na kuongezeka kwa mtaji.
Akizungumzia mafanikio ya benki tanzu za Exim zilizopo katika nchi tatu: Komoro, Djibuti na Uganda,
Bw. Ponda alisema kuwa Komoro na Djibuti wamefanya vizuri na kuweza kupata faida mara 3 ya mwaka
uliopita na kufikia Tsh bilioni 8 kutokana na ukuaji mzuri wa uchumi na huduma bora. Na benki tanzu
mpya ya Uganda ilipata hasara ndogo ya Tsh milioni 177, na inategemewa kufanya vizuri zaidi mwaka
huu baada ya kuteleza mikakati mipya baada ya Benki ya Exim kununua hisa zaidi ya 58.6%.
Notes to Editors
About EXIM Bank:
EXIM Bank (Tanzania) Limited was established in 1997 and expanded its market by opening subsidiaries
in Comoro (2007), Djibouti (2010) and Uganda (2016), hence became the first local bank to go offshore.
Its core objective is to create investment value to its shareholders and optimize the growth through
delivery of customized services. Along with this, the Bank is well known to deliver excellence by serving
customers with efficiency and courtesy.
Within a short span of 20 years of its existence, the bank has built a strong brand through its
geographical reach, innovative products, relationship management and its ability to provide a faster
turnaround in services and in the process building a strong loyal customers base.
The Bank has 29 branches (including 2 mini branches) & 57 ATMs within in Tanzania. Overall the Bank
0 maoni:
Chapisha Maoni