TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
UJENZI WA MTO LWAMPULA KUIMARISHA USAFIRISHAJI WA MIZIGO TOKA TANZANIA KWENDA DRC
Gavana wa Jimbo Katanga Jean Claude Kazembe amesema kuwa ili urahishaji wa ujenzi wa daraja katika mto Lwapula uliopo katika mpaka wa Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) utasaidia kurahisha usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kwenda Jimbo la Hault Katanga DRC.
Gavana huyo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya ziara yake katika Badari ya Dar es salaam.
Alisema kuwa endapo nchi za Zambia na DRC zitakubaliana kujenga Daraja hilo, kutaimarisha biashara pamoja na kukuza uchumi wa nchi za Tanzania, DRC na Zambia kwa kuwa itachukua muda mfupi kwa Wasafirishaji wa Mizigo kutoka Dar es salaam kwenda DRC.
“Kujengwa kwa daraja hilo kutarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka nchini Tanzania kwenda nchini DRC, na hivyo kufanya gharama za usafirishaji wa mizigo kupungua” alisema Gavana Kazembe.
Gavana Kazembe aliongeza kuwa daraja hilo litakalogharimu dola milioni 85 litakalikuwa na urefu wa mita 700 linatarajiwa kujengwa kwa ushiririkiano wa Serikali za nchi za Tanzania, Kongo na Zambia kwa vile litanufaisha nchi hizo kiuchumi.
Aidha, Gavana Kazembe alisema kuwa atajitahidi kushauri Serikali hizo zijenge daraja katika mto Lwapula ili kusaidia Bandari ya Dar es salaam kuendelea kutoa huduma nzuri za usafirishaji wa mizigo kati ya Dar es Salaam na Kongo.
Aidha, alisema kuwa katika mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alifurahishwa na hatua hiyo kwa kuwa itasaidia kukuza urafiki uliopo baina ya Tanzania na Kongo pamoja na kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kwa gharama nafuu.
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA, 80 WATIWA NGUVUNI ARUSHA
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wiki chache baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kukamata gunia 58 za bhangi ambazo ziliteketezwa kwa moto na kuharibu hekari 31 za mimea ya zao hilo katika maeneo ya Kismiri Juu na Engalaon wilayani Arumeru, Jeshi hilo limeendelea na misako dhidi ya wauzaji, watumiaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa 80 katika misako iliyofanyika kwa muda wa siku 4 tu.
Akitoa taarifa hiyo leo asubuhi ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba misako hiyo imefanikisha kukamata jumla ya kete 167 za madawa ya kulevya aina ya Heroin pia misokoto 3,845 ya Bhangi na mirungi kilogramu 33.
“Katika misako hiyo ambayo ilifanyika wilaya zote sita za mkoa huu, watuhumiwa 54 walipatikana kwenye tuhuma za Bhangi, 14 ni tuhuma za Heroin na 12 ni wa tuhuma za mirungi.” Alisema Kamanda Mkumbo.
“watuhumiwa 40 ni wauzaji wa madawa hayo huku 13 ni wale ambao walikuwa wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na Bhangi na mmoja alikuwa anasafirisha, watuhumiwa 14 wa Heroin kosa lao kupatikana huku 12 makosa yao ni kupatikana na mirungi na hivyo kufanya idadi yao kuwa 80 ambao ni wanaume na wanawake”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.
Kamanda wa Polisi aliwashukuru wananchi wa mkoa huu kwa ushirikiano wa utoaji wa taarifa za uhalifu na kuwaomba waendelee kufanya hivyo na kutoa onyo kwa wale wachache wanaojihusisha na uhalifu wa namna hiyo waache mara moja vinginevyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionyesha baadhi ya kete za Heroin ambazo zilikamatwa hivi karibuni kutokana na misako inayoenndelea mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
NEC: KUIZUIA KADI YA KUPIGIA KURA YA MTU MWINGINE NI KINYUME CHA SHERIA
Hussein Makame, NEC aliyekuwa Bukoba
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewatahadharisha watu wanaochukua kadi za kupigia kura za wenzao na kuzizuilia au kubaki nazo kuwa ni kinyume cha Sheria.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba na Shinyanga hivi karibuni.
Alisema kifungu cha 88 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinasema kuwa ni kosa la jinai kwa mtu kuchukua kadi ya mpiga kura mwingine na kuiziulia, kukataa kuirudisha au kubaki nayo kwa uzembe.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Jaji Richard Kibela baada ya mwenyeji wake kumpokea wakati akiwasili mkoani Shinyanya kutoa Elimu ya Mpiga Kura mkoani humo.Kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga Sekela Mwaiseje.
Bw. Kawishe alifafanua kuwa kumekuwa na malalamiko kwamba inapofikia karibu na kipindi cha uchaguzi, baadhi ya watu wanachukua kadi za wapiga kura wengine na kuzizuia kinyume cha Sheria.
Hata, hivyo alisema kutokana na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia mikutano na kuhudhuria maonesho mbalimbali, baadhi ya wananchi wameelewa umuhimu wa kadi hizo na kuahidi kutoampa mtu kadi zao za kupigia kura.
“Kwa hiyo katika jambo hilo tumekuwa na mrejesho ambo ni chanya lakini tunachowaomba ukiandikishwa tunza kadi yako ya mpigia kura” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa; “Jambo la pili mwananchi usikubali mtu achukue kadi yako ya mpigia kura na wala usitumie kadi yako ya mpiga kura kwenye kuchukulia dhamana sehemu yoyote”
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akisamiliana na Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bw. Geofrey Ramadhani Mwangulumbi baada ya kuwasili kwenye Halmashauri hiyo kutoa Elimu ya Mpiga kura.
“Kwa sababu itakwenda kuchukulia dhamana alafu utashindwa kwenda kupiga kura unapofika wakati wa kupiga kura, mwananchi ajue kwamba kupiga kura ni haki yake” Alisema mtu aliyejiandikisha asipokwenda kupiga kura anakosa haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka na badala yake anawaacha wenzako wakuchagulie kiongozi.
“Unaacha kupiga kura alafu baadaye anakuja kulalamika unasema huyu kiongozi simtaki kumbe kura moja inatosha kubadilisha matokeo ya eneo zima” alisema.
Hivyo aliwasihi wananchi waendelee kuzingatia amani katika uchaguzi na kuwashukuru kwa jinsi uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22 mwaka huu kwa jinsi ulivyokuwa na amani na utulivu.
”Kwa kweli Watanzania tutambue kuwa amani ni yetu sisi sote na sisi ndio tutakaoilinda hiyo amani tuiweke Tanzania yetu kwanza alafu sisi baadaye” aliwakumbusha Watanzania.
Akijibu swali la mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bukoba aliyehoji anayepoteza kadi ya mpiga kura anachukuliwa hatua gani kumuwajibisha, Bw. Kawishe alisema hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yake.
Alifafanua kuwa wale wote wanaopoteza kadi ya mpiga kura wanatakiwa wafike kwenye kituo cha uboreshaji wa daftari la wapiga kura na kujieleza na watapatiwa kadi nyingine.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati alipomtembelea ofisini kwake mkoani humo.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe akitoa Elimu ya Mpiga kura kupitia Kituo cha redio Faraja Fm cha mkoani Shinyanga mwishoni mwa wiki hii.Kulia kwake ni mtangazaji wa redio hiyo Faustin Kasala.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa Elimu ya Mpiga kura kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Old Shinyanga iliyopo manispaa ya Shinyanga. Picha na Hussein Makame, NEC
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
BILIONI 18 KUTUMIKA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI DAR
Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) inatekeleza mradi wenye thamani ya bilioni 18 unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa ufundi na uendeshaji wa Mamlaka hiyo Bw. Romanus Mwangingo wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika eneo la Kimbiji ambako ndipo mradi huo unapotekelezwa .
“Mkandarasi anaendelea na kazi na ameleta mabomba yote na amechimba visima 15 na vitazalisha maji yatakayotumika katika Jiji la Dar es salaam na mradi unatarajiwa kukamilika machi 2017” Alisisistiza Mwangingo. Aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 85 na utakapokamilika maeneo ya Kigamboni,Temeke,Ilala na Jiji la Dar es salaam kwa ujumla yatanufaika kwa kupata huduma ya maji.
Maji yakitoka kwenye moja ya Kisima Kirefu kilichochimbwa katika eneo la Kimbiji unakotekelezwa mradi mkubwa wa unaolenga kutatua changamoto ya maji katika Jiji la Dar es salaam.
Kwa upande wa miradi mingine kama ule wa ujenzi wa Bomba kutoka Ruvu juu hadi kimara Mwangingo amesema ulikamilika mwezi oktoba 2016 na uzalishaji wa majaribio unaendelea.
Mradi huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 59 ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuhakikisha kuwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam wanapata huduma ya maji safi na salama. na kuondokana na changamoto hiyo. . Aidha mradi huo utawezesha kiwango cha maji kufikia lita milioni 196 kwa siku kutoka lita milioni 82 za awali.
Kwa upande wake Bw.Salum Hamis mkazi wa mbagala amepongeza miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi kwa kuwa imekuwa chachu ya maendeleo katika maeneo yao. Aliongeza kuwa miradi hiyo imechochea kupunguza tatizo la maji na imewawezesha wananchi kutumia muda mwingi katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.
Meneja Uhusiano wa DAWASA Bi Neli Msuya akieleza kwa waandishi wa habari faida za miradi inayoibuliwa na Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam.
Katika kukabilina na tatizo la miundombinu ya maji taka katika Jiji la Dar es salaam mamlaka hiyo iko katika mchakato wa kuanza ujenzi wa mtambo mkubwa wa kuchuja maji taka katika eneo la Jangwani na kuboresha mfumo wa maji taka katikati ya Jiji.
Mradi mwingine ni ule wa upanuzi wa ruvu chini ambao umekamilika kwa asilimia mia moja na utawezesha upatikanaji wa maji kufikia lita milioni 270 kwa siku kutoka milioni 180 kabla ya mradi huo haujatekelezwa.
Majukumu ya DAWASA ni kumiliki miundombinu ya maji safi na maji taka kwa niaba ya Serikali, kusimamia utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka Dar es salaam, kugharimia,kupanga mipango na kusimamia upanuzi wa huduma na kuishauri Serikali kuhusu masuala ya huduma ya maji safi na maji taka Jijini Dar es salaam.
Mtambo unaotumika kuchoronga Visima Virefu ukiwa katika eneo la Kimbiji unapotekelezwa mradi mkubwa wa uchimbaji visima virefu.
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
KURA HAZIIBIWI MAHALI POPOTE SIKU YA UCHAGUZI
Na Bartholomew John Wandi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawawahakikishia Umma wa Watanzania kuwa hakuna kura yoyote inayoibiwa sikuwa ya kupiga kura, iwe Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani au Uchaguzi Mdogo wa Ubunge au Udiwani.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchagzi, Kailima Ramadhan Kombwey wakati alipokutana na Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Pulisher waliotaka kujua Mchakato wa Uchaguzi hadi kuhesabu kura na kumtangaza Mshindi.
Watu wengi vikiwamo vyama vya Siasa huwaminisha Wafuasi wao kuwa wakati wa kupiga kura huibiwa kura zao ndiyo maana huwashawishi wafuasi wao kulinda kura zao kitu ambacho hakipo
Mkurugenzi alieleza kuwa Kabla ya siku ya Kupiga Kura, Vyama vyote vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wao wa Urais,Ubunge na Udiwani huagizwa kuleta Mawakala wao wa Kulinda kura zao na maslahi ya Vyama vyao vya Siasa na kuwa makini na mchakato unavyoendelea Kituoni.
Mara nyingi Mawakala wanatakiwa kutoka katika maeneo wanayoishi ili kubaini mtu ambaye hawamfahamu asiweze kupiga kura kwa kutumia kadi ya mtu mwingine.
“Baada ya Mpiga Kura Kumpa Kadi ya Kupigia Kura, Msimamizi wa Msaidizi wa Kituo baada, hutafuta jila la Mpiga Kura huyo na anapoliona hulisoma kwa sauti kubwa ili Mawakala wa Vyama nao wasikie na kuhakikisha anayeitwa jina hilo ndye mwenyewe au siye?” alisema Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Kama anayeitwa jina ndiye Mpiga Kura Mwenyewe huruhusiwa kuendelea na Mchakato wa Upigaji kura lakini kama Mawakala wakiona siye mwenye jina hilo na wana ushahidi wa kutosha humzuia asipige kura.
Mara nyingi pia baadhi ya mashabiki na wafuasi wa Vyama vya Siasa huvumisha kuwa watu waliokufa majina yao wameonekana yametikiwa kuonyesha kuwa jina lake limetumiwa na mtu mwingine kupiga kura kuonyeha kuwa sio kweli kwa sababu Mawakala wa Vyama hivyo vya Siasa wangembaini.
Mkurugenzi alibainisha kuwa siyo jambo jema kwa Wakala wa Chama cha Siasa kukataa kusaini Matokeo ya Uchaguzi ya awali yanapotangazwa kituo cha Kupigia Kura, Kwenye Kata baada ya Kujumlishwa na Kumtanga Mshindi wa Udiwani au Jimboni anapotangazwa Mshindi wa Ubunge au au Makao Makuu ya Tume anapotangazwa Mshindi wa Urais kwa sababu kwa sababu muda wote alishiriki hatua zote na hajaona mahali popote alipoona aliibiwa kura.
Aidha, Murugenzi alisistiza kuwa kutosaini kwa Wakala wa Chama hakumzuii Mwenyekiti wa Uchaguzi kutomtangaza Mshindi wa Kiti cha Urais, Msimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo kutomtangaza Mshindi wa Kiti cha Ubunge au Msimamizi Msaidizi Ngazi ya Kata kutomtangaza Mshindi wa Udiwani.
“Pamoja na hayo, hakuna hata siku moja Mawakala wa Vyama vya Siasa waliowahi kuleta ushahidi wao wa Matokeo ya awali vituoni Tume na kulalamika kuwa matokeo yaliyotangazwa ni tofauti na niliyo nayo”. Alisema Kombwey.
Mkurugenzi wa Uchaguzi alimalizia kwa kuwapa Wafanyakazi wa Global Publisher nafasi ya kufanya onyesho la Upigaji Kura Kituoni kwa kushiriki wenyewe nafasi zote kuanzia Mawakala, Msimamizi wa Kituo, Msimamizi Msaidizi wa Kituo na Wapiga Kura, Ujumlishaji wa Kura za Awali Kituoni za Ubunge Mpaka Jimboni na Kumtangaza Mshindi wa Kiti cha Ubunge.
Wafanyakazi hao wa Global Publisher walipata kufahamu kuwa Mchakato wote waliofanya Kituoni hakuna mwanya wowote ulioonekana kwa Chama Chochote cha Siasa kuiba Kura au kuibiwa kura au Mtu ambaye siyo wa Kituo hicho kuruhusiwa kupiga Kura.
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke aliyefika Ikulu kwa ajili ya Mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay Ikulu jijini Dar es Salaam.
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
ALICHOKIONGEA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017 ~
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA ZIARANI SINGIDA KUTEMBELEA VITUO VYA WAZEE WASIOJIWEZA
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.
Wake hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.
Wameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Katika kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi.
Akizungumza na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka eneo hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na hakikisheni kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.
Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.
“Watanzania wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo na hiki tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada mbalimbali kkwa kadri tutakavyojaaliwa,” amesema.
Awali Mkuu wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida.
Bw. Ngoo alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja huku mahitaji yakiwa ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na zina nyufa.
Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na Bibi Agnes Kamota (75) walipomtembelea nyumbani kwake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitembelea Zahanati ya Sukamahela katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa msaada wa vyakula tani 7.5 katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msaada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa tawi la Benki ya NMB Singida Bw. Abius Mlengwa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa Tawi la CRDB Manyoni Bw. Richard Karatta katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017. PICHA NA IKULU.
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
WANAHABARI WATAKIWA KUACHA KUAMINI KILA KITU, WASOME
SERIKALI imewataka wanahabari kusoma sheria, taratibu na kanuni zinaogusa tasnia yao ili iweze kuendelea na kuachana na kuamini kila kitu wanachoambiwa na mtu mmoja.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati akizungumza katika siku ya radio duniani, hafla iliyofanyika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.
"Watu someni sheria, taratibu na kanuni kwa kina ili kujua na kuzielewa, mkielewa kama kuna sheria inakwaza ukuaji wa sekta ya habari tuseme tukae chini.. " alisema Waziri Nape akijibu hoja kuhusu sheria za habari zilizopo ambazo zinadaiwa kukwaza uhuru wa ukusanyaji wa habari.
Ilielezwa katika hafla hiyo kuwa sheria za sasa ya takwimu na habari zinakwaza uhuru wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Katika hoja hiyo Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA) Prosper Kwigize katika hotuba yake kwa Serikali, alisema kwamba redio hizo zinachangamoto nyingi katika utendaji wake ikiwamo sheria zilizopo,watoa habari wasioeleweka na wanazuia upatikanaji wa habari.
Nape alisema kwamba sheria si msaafu na kwa kuwa asilimia 80 za habari zinazalishwa na serikali, waandishi wanahaki ya kupata habari hizo na kama kuna kikwazo ni lazima kitafutiwe suluhu.
"Tukae tushindane kwa hoja tukubaliane na kuhakikisha kwamba tunarekebisha.. Bunge kazi yake ni kutunga na kufuta sheria" alisema Nape ambaye alisema kwamba sheria ya sasa imetoa nguvu kwa watoa habari na kwamba si kila habari iliyopo serikalini ni classified.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (wa pili kulia) akimpongeza Meneja wa Redio Jamii Orkonerei FM, Baraka David Ole Maika baada ya kuwasilisha risala ya mafunzo ya ufundi kwa Redio za Jamii wakati maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam jana. Kulia Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi, Wa tatu kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Wanne kulia Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka na Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper Kwigize.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akisheheresha kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya radio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues akitoa neno la ukaribisho liliombatana na ujumbe maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
RC MAKONDA AMSHAURI SPIKA WA BUNGE,NDUGAI KUWAPIMA WABUNGE KUBAINI NAO KAMA WANATUMIA DAWA ZA KULEVYA AMA LA.
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBURUARY 14,2017
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
WADAU NKAINA NA BI REHEMA WA DALLAS, TEXAS WAMEREMETA HUKO MIAMI, FLORIDA USA
Wadau Bw. Nkaina na Bi Rehema wa Dallas, Texas wakiwa na nyusoza furaha sana baada ya meremeta huko Miami, Florida USA, Jumapili
Bibi Harusi akiwa Na mwanae Jr Mazara
Maharusi wakiwa Na wapambe wao
Maharusi wakifurahia siku yao ya siku
TUESDAY, FEBRUARY 14, 2017
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
RC MAKONDA AKABIDHI ORODHA YA MAJINA 97 YA WAUZA DAWA YA KULEVYA KWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DAR LEO
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akionyesha majina mengine 97 ya wauza Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa Bw. Rogers William Sianga Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ili yaanze kushughulikiwa. RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya pili iliyoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kuendelea mpaka awamu ya sasa ya Rais Dkt John Pombe Magufuli, , Katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNCC.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikabidhi majina mengine 97 kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa Bw. Rogers William Sianga, kuwa ili yaanze kushughulikiwa.RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya pili iliyoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kuendelea mpaka awamu ya sasa ya Rais Dkt John Pombe Magufuli, , Katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNCC.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza katika mkutano huo,ambapo amekabidhi majina mengine 97 ya awamu ya tatu kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,Bw. Rogers William sianga ili yaanze kushughulikiwa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza jambo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers William Sianga katika mkutano maalum wa kutoa tathmini ya kampeni ya kutokomeza biashara haramu ya madawa ya kulevya katika mkoa wa Dar es salaam na nchi nzima kwa ujumla.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Khaleed Mohammed almaarufu TID akitoa ushuhuda wa namna alivyokuwa akitumia Dawa za kulevya,na sasa amekiri hadharani kuacha kutumia na kuunga mkono juhudi za kupambana na Dawa za kulevya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Khaleed Mohammed almaarufu TID akitoa ushuhuda wa namna alivyokuwa akitumia Dawa za kulevya,na sasa amekiri hadharani kuacha kutumia na kuunga mkono juhudi za kupambana na Dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Saimon Sirro akizungumza wakati akitoa taarifa ya kampeni hiyo leo.
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017 ~
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
ALICHOZUNGUMZA KAMANDA SIRRO LEO JIJINI DAR KATIKA HARAKATI ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
KIPINDI MAALUM HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI BAADA YA KUMUAPISHA KAMISHNA WA DAWA ZA KULEVYA
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
ORODHA YA MAHAKIMU NA MAJAJI WALIOVURUGA KESI ZA WAUZA UNGA KUTUA KWA JAJI MKUU
Na Torinto Hot Media.
JAJI Mkuu anatarajia kupokea orodha ya majina ya mahakimu na majaji ambao wanadaiwa kuvuruga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Hayo ameyasema leo Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga wakati wa mkutano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili kupambana na dawa za kulevya.
Sianga amesema kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote watakaobainika kuhusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo wamezipata kwa biashara hiyo zitataifishwa.
Amesema kuwa watazunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi orodha ya majina 97 wanaojihusisha na dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto umewashwa dhidi ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.
Amesema kuwa kuna nyumba 200 zinajihusisha kufanya biashara ya madawa ya kulevya hapa jijini ambapo wote hao watafikiwa katika operesheni,ambayo mojawapo wanatarajia kuifanya usiku wa leo.
Nae Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed almaarufu kwa jina la kisanii TID , amesema kuwa sasa ni mnyama ambae yuko tayari kupambana na watu wanaouza pamoja na kutumia dawa za kulevya na amerudi kwa kufanya kazi na kuongeza kuwa kuimba hakuitaji dawa za kulevya.
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
JAJI FATUMA HAMISI MASENGI AAGWA RASMI MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA LEO
Na.Torinto Hot Media
Sherehe za kumuaga aliyekuwa Jaji mfawidhi wa mahakam kuu kanda ya Arusha Mhe,Fatuma Hamis Masengi ,zimefanyika leo katika mahakama kuu ya ndanda hiyo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo majaji,mahakimu,mawakili wasajili wa mahama watendaji pamoja na wageni waalikwa.
Sherehe hizo zimeanza majira ya saa asubuhi katika mahakama ya wazi ambapo Jaji Fatuma alianza kufanya kazi mnamo mwaka 1974 katika mahakama ya mwanzo na kuendelea kuitumikia mahakama hadi alipoteuliwa kuwa jaji mfawidhi mahakama kuu.
Amewataka majaji na mahakimu pamoja na wale wote wanaofanya kazi za kimahakama wafanye kazi kwa kumtegemea Mungu huku wakijua kazi yeyote ina changamoto zake hivyo ni vyema kufanya kazi kwa weledi zaidi na kwa kuzingatia sheria inavyosema,wakimtendea haki kila mtu kwa stahiki.
Amewataka wanawake kutokukata tamaa huku akisema kuwa wanawake wanaweza kuliko wanaume japo kuwa wakati mwingine wanaume wanaona kama vile wanawake ni wanyonge lakini mwanamke anaweza pale ambapo anasimama kwa nafasi yake na kulitumikia kusudi kwa wakati na weledi.
Mhe.Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi
Picha ya pamoja kati ya waheshimiwa majaji kanda ya Arusha na Kilimanjaro ,Wakwanza kulia ni mhe,Jaji Dkt.Modesta Opiyo,Wakwanza kushosto ni mhe,Jaji Salma Maghimbi,akifuatiwa na aliyeko kushoto kwake mhe,Jaji Sekela Mushi,akifuatiwa na mhe,Jaji mstaafu Fatuma Hamis Masengi wakiwa na majaji wengine pamoja na waheshimiwa mahakamu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Picha ya pamoja ya waheshimiwa majaji pamoja na mawakili wa serikali,na wale wa kujitegemea.Picha na Vero Ignatus Blog.
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
WANAHABARI TUMUUNGE MKONO RAIS KATIKA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amevishauri vyombo vya habari nchini kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo Kikuu huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa vyombo vya habari viwe sehemu ya kuwaunganisha watanzania katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
“Wanahabari tuliunganishe taifa letu tuwe kitu kimoja katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya” alisisitiza Mhe. Nnauye.
Ameongeza kuwa sasa ni wakati wa watu wote kuungana kwa pamoja zikiwemo tasnia zilizopo katika Wizara yake za Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwani vita hii ni ya watanzania wote na sio mtu mmoja au Serikali pekee.
Aidha Mhe. Nape amevitaka vyombo vya habari kutobaki nyuma katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na kuhakikisha haki inatendeka na vita dhodi ya madawa ya kulevya vinashinda.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau Redio na vyombo vya habari kwa ujumla katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
MONDAY, FEBRUARY 13, 2017
MAAFISA HABARI NA TEHAMA KUTOKA MIKOA MITANO WAPIGWA MSASA
SERIKALI imewataka Maafisa Habari na Maafisa Tehama katika sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini kuweka taarifa sahihi zenye kuzingatia muda na wakati ili kuongeza ufanisi wa kutangaza shughuli za Serikali kwa umma.
Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Katibu Tawala wa Mkoa huo, C.P Clodwig Mtweve, katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi, Johnsen Bukwali wakati wa mafunzo elekezi ya uwekaji wa taarifa katika tovuti yaliyoandaliwa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Umma (PS3) kwa Maafisa Habari na Tehama wa Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu.
Kwa Mujibu wa C.P Mtweve alisema uwekaji taarifa katika tovuti hizo zitasaidia kuimarisha shughuli za utawala na kuifanya Serikali kufahamika zaidi kwa wadau wake na hivyo kupunguza malalamiko ya mara kwa mara yanayotolewa na wananchi kuhusu huduma zake kwa umma.
“Ninyi ndio mmekuwa wachakataji wa taarifa za Serikali na kuhakikisha zinaufikia umma wa Watanzania zikiwa katika hali ya ubora kwa kutumia njia mbali mbali za mawasiliano kama vile mbao za matangazo na hata kwa njia ya mitandao” alisema C.P Mtweve.
Kwa mujibu wa C.P Mtweve alisema kuwa lengo la Serikali ni kuongeza uwazi na wigo wa upatikanaji wa taarifa sahihi na zenye uhakika katika tovuti zake ili kuiepusha Serikali na habari za kuzusha na zisizo na maslahi kwa taifa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebecca Kwandu akizungumza na wajumbe wa kikao cha mafunzo ya Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mwanza. Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Johnsen Bukwali.
Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma, Desderi Wengaa akizungumza na wajumbe wa kikao cha mafunzo ya Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mwanza. Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Johnsen Bukwali
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mwanza, Johnsen Bukwali katikati (walipokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo elekezi kwa Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Hallmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kagera na Mara mara baada ya kufungua mafunzo hay oleo Jijini Mwanza.
0 maoni:
Chapisha Maoni