Mauzo ya Soko
Mauzo yameshuka kutoka TZS 13.2 Bilioni hadi TZS 5.5 Billion.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imepungua kutoka hisa 2.8 millioni hadi hisa laki 5.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
TBL ………………………………………..98.3%
TCC ………………………………………. 0.7%
NMB …………………………………….. 0.6%
Ukubwa wa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umeongezeka kwa takribani shilingi 500 Bilioni kutoka Shilingi Trilioni 18.6 hadi Shilingi Trilioni 19.1
Mtaji wa kampuni za ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha Shilingi Trilioni 7.5
Viashiria (Indexes)
Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yani DSEI kimepanda kwa pointi 53 kutokana na ongezeko la bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.
Kiashiria cha kampuni za ndani kimeendelea kubaki kwenye wastani wa TZS 3,550 wiki hadi wiki.
Sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa TZS 4,508 wiki hadi wiki.
Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa TZS 2,644.
Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa TZS 3,158.
Hati Fungani
Mauzo ya hati fungani yamepanda kwa asilimia 30% kutoka Shilingi 131.8 Milioni kufikia Shilingi 172 Milioni.
Hati fungani mbili za serikali zenye thamani ya Shilingi 76 Milioni na hati fungani moja ya EXIM yenye thamani ya Shilingi 96 Milioni ziliuzwa na kununuliwa wiki hii iliyoisha tarehe 13 Januari 2017.
0 maoni:
Chapisha Maoni