Na Jerome Mlaki wa Dar. 0789106710
Soko la kariakoo jijini Dar es salaam.. limezindua kituo Cha huduma Kwa wateja chenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wateja lakini ikiwemo pia kurahisisha upatikanaji wa taarifa za kibiashara ndani na nje ya soko.
Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi huo mgeni rasmi Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Selemani amesema Makampuni mbalimbali pamoja na wateja na wafanyabiashara watanufaika na huduma hiyo kwani inarahisisha mawasiliano ya kiutendaji na utatuaji wa kero mbalimbali katika soko hilo.
Makampuni mbalimbali pamoja na wateja wameuongelea Uzinduzi huo na kusema ni urahisishaji wa mawasiliano ya kibiashara lakini pia ni sehemu maalumu ya kuuliza chochote ili kupata taarifa zaidi badala ya wageni wengi kuzubaa wa kuteseka namna ya kufahamu maeneo zilipo bidhaa.
Ikumbukwe kuwa soko la kariakoo liliungua kabla ya kujengwa jipya hivyo wafanyabiasha wa soko hilo walipitia changamoto mbalimbali ikiwemo sehemu ya kufanyia biashara lakini pia uduni wa upatikanaji wa bidhaa, hata wateja wao kukosa bidhaa mara nyingi walipofika katika mazingira hayo.
Lakini Kwa sasa baada ya kukamilika soko hili la kariakoo wafanyabiashara wamemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Kwa kutatua changamoto yao ya muda mrefu.
Na Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo, CPA Ashiraph Abdulkarim amesema Kituo Cha huduma Kwa wateja chenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wateja na wafanyabiashara pamoja na kupata taarifa zaidi kuhusiana na soko kimezinduliwa ili sasa kuwaweka watu wote karibu kibiashara.
Mara baada ya kuzindua kituo hicho mgeni rasmi Bi. Charangwa Selemani amesema sasa wakati wa wafanyabiashara kurahisishiwa utatuaji wa kero zao umefika na kurahisishiwa upatikanaji wa taarifa za kibiashara ndani na nje ya nchi umefika.
Mgeni rasmi Bi. Charangwa Selemani amesema kituo hicho kimeyengeneza fursa zaidi na hivyo hata wateja hawatababaika Tena wapi waulize ili wapate taarifa muhimu za soko moja kwa Moja wateja hao watapiga namba 0800114040 na kueleza shida na kujibiwa.





0 maoni:
Chapisha Maoni