WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 7 Desemba 2023

 22:39      No comments

  Digital Online

Torintohot Hot 

Na Joseph Liemi


MWENYEKITI wa Baraza la Chuo Kikuu Ardhi, Balozi Salome Sijaona ametoboa siri ya mafanikio ya Chuo hicho kusika nafasi ya kumi bora miongoni mwa vyuo 120 Barani Afrika.





Hayo yalijiri juzi wakati wa mahafali ya 17, ya chuo hicho yaliyofanyika katika viunga vya chuo hicho mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya halaiki ya watu.



“Chuo chetu kimeshika nafasi ya kumi kati ya vyuo mi ana ishirini Afrika Kusini n mwa Jangwa la Sahara kwa mwaka 2023 kati ya vyuo 120 vilivyoshindanishwa ushindi huo siyo tu umezidisha kupeperusha jina la chuo kikuu ardhi katika medani za dunia kitaaluma bali chuo kimeendelea kujitangaza hasa kwenye maeneo ambayo chuo kina ubobezi” alisema Salome.



Kwa mujibu wa Salome siri ya mafanikio hayo yametokana na sera, miongozo mbalimbali itolewayo na serikali, hati idhini ya chuo na baraza la chuo chini uongozi wa Balozi Salome vimekuwa ni ngao imara kwao kuhakikisha maamuzi mbalimbali ya kimaendeleo yanafanyika kwa mustakabali wa chuo hicho.



Aidha Balozi alikipongeza chuo kwakutoa elimu thabiti kwa wahitimu na wanaoendelea na masomo kwakuendelea kuvumilia changamoto za chuo na kusoma kwa bidii ili kufanikisha malengo waliyojiwekea.









Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo , Profesa Evaristo Liwa alisema Jumuiya ya chuo inaahidi kuendelea  kutoa  ushirikiano kwa viongozi wote ili kuhakikisha taifa linafikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya 2025 ya kuwa na Maisha bora kwa kila mtanzania, amani, umoja, utawala bora, taifa lililo elimika  na lenye uchumi shindani na endelevu kwa manufaa ya watu wote.





“ Naomba sasa niwageukie ma profesa ,wahadhiri,  na watumishi wote wa chuo hiki, mfahamu yakwamba nyinyi ni nguzo muhimu hasa katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku na kuwahudumia wanafunzi wetu waliopo na wanaohitimu hii leo,, niwaombe muendelee kufanya kazi kwa bidi, ushirikiano na juhudi ili kukiletea chuo chetu jina zuri mbele ya uso wa Taifa.













Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 1,148 walitunikiwa  shada mbalimbali  ambapo 1,117 walitunikiwa vyeti vya shahada ya awali, 27, shahada za uzamili,  na wa 4 shahada za uzamivu.












Idadi ya wanafunzi wakiume ni 639 sawa na asilimia 55.7 na wakike ni 509 sawa na asilimia 44.3 ni matumaini ya wazazi, walezi na taifa kwamba wahitimu hao watatumia vyema elimu waliyoipata kwa manufaa yao na Taifa.






0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *