Mamia ya wakazi wa mji wa Musoma mkoani Mara wamejitokeza kuaga na kushiriki mazishi ya mapacha wawili wanafunzi wa chuo cha Mipango Kampasi ya Mwanza waliofariki dunia baada ya kuzama Ziwa Victoria walipokuwa wanaogelea.
Musoma. Miili ya pacha wawili ambao walikuwa ni wanafunzi wa Chuo cha Mipango Kampasi ya Mwanza imewasili katika Kanisa la Katoliki la Bweri, Manispaa ya Musoma kwa ajaili ya misa ya mazishiapacha hao Kenny na Lenny Makomonde (24) waliofariki dunia baada ya kuzama Ziwa Victoria Jumapili Mei 28, 2023 saa 12 jioni walipowenda kuogelea katika ufukwe wa Mihama Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa ratiba mapacha hao wanatarajiwa kuzikwa leo Jumanne Mei 30,2023 nyumbani kwao Bweri katika Manispaa ya Muso
Maandalizi ya mazishi yanaendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa makaburi watakayozikwa mapacha hao.
Miili ya mapacha hao iliwasili nyumbani kwao Bweri Manispaa ya Musoma usiku wa kuamkia leo baada ya ibada na taratibu zingine kukamilika jijijini Mwanza jana.
Baada ya kuzama majini miili ya pacha hao iliopolewa Mei 29,2023 kwa ushirkiano kati ya wananchi na kikosi cha Zimamoto cha Mkoa wa Mwanza baada ya jitihada za kuitafuta kwaajili ya uopoaji siku ya tukio kushindikana kutokana sababu mbalimbali ikiwemo giza.
Mapacha hao ambao walikuwa mwaka wa tatu katika chuo hicho walikuwa wakisomea kozi ya Mipango na Maendeleo
0 maoni:
Chapisha Maoni