Torinto hot media blog
Na Jerome Mlaki wa DAR
Waziri wa Maji mheshimiwa Jumaa Aweso akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi kuchepusha maji kutoka katika bomba kuu la Ruvu chini eneo la Tegeta Wazo kwaajili ya kuyatawanya maji katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akizungumza na waandishi wa habari
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja akifafanua namna dawasa ilivyojipanga kuakikisha kuwa inapunguza mgao wa maji jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maji mheshimiwa Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Maji na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (Dawasa) kuhakikisha wanazingatia ratiba za mgao wa maji walioutangaza.
Waziri Aweso amesema hayo alipotembelea kujionea kazi ya kuchepusha maji kutoka katika bomba kuu la Ruvu chini eneo la Tegeta Wazo jijini Dar es Salaam jana, kwaajili ya kuyatawanya maji katika maeneo mbalimbali ya jiji unaofanywa na Mamlaka ya Maji na Usafiri wa Mazingira (Dawasa), eneo la Tegeta Wazo.
Amesema wizara kwa itashirikiana bega kwa bega na Dawasa katika kipindi hiki ambacho wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wameanza kupata maji kwa mgao kutokana na ukame uliosababisha kupungua kwa maji katika mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu kutokana na ukame wa mvua.
"Napenda kutoa pongezi za dhati kwa na kushukuru viongozi wa mkoa kwa ushirikiano wao na Dawasa kuhakikisha katika kipindi hiki cha mpito wanakuwa pamoja," Alisema Aweso.
Alisema ratiba ya mgawo wa maji iliyotolewa ni muhimu ifuatwe bila kuwepo na upendeleo husussani katika kipindi hiki ambacho utoaji wa maji umepungua na uwezo wetu ni lita milioni 320 kwasasa tunazalisha lita milioni 300.
Aidha Waziri Aweso ameiomba Dawasa kushirikiana na watu wenye visima vikubwa ili kurahisisha upatikanaji wa maji katika kipindi chote cha mgao
Pia waziri aweso aliongeza kuwa tayali hatua mbalimbali zomeshaanza kuchukuliwa kuhakikisha upatikanaji wa maji unaendelea kuwepo kwa ujenzi wa visima vya kigamboni ambavyo vitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 70 mpaka Jumapili utakuwa umekamilika na itasaidia kupunguza makali ya shida ya maji.
"Tayali tuna ujenzi wa bwabwa la Kidunda ni makakati wa muda mrefu zaidi ya miaka 50 tumeshapata mkandarasi atajenga bwawa hilo," aliongeza waziri Aweso.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe ametoa wito kwa wananchi kutolalamika atika kipindi hiki kwani miradi iliyopo ni endelevu kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji.
“Serikali imekuwa ikijenga mradi wa muda mrefu wa maji wa mabomba yayotasahimili presha kubwa ya maji na yatakaosaidia katika usambazaji wa maji mpaka Desemba utakuwa umekamilika na maji hayatakuwa changamoto,” Alisema Gondwe.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja amemshukuru Waziri Aweso na kusema changamoto ya maji ipo lakini tayari wameshaanza kuitatua ili kuwezesha maji kupatikana katika maeneo ya Bunju, Mbweni, Salasala, Mbezi na Songawima na Madale.
Alisema tayali wamechukua tahadhari za haraka kwa kujenga mradi wa kigamboni ambao utaweza kupunguza changamoto ya mgao wa maji na tayali mhandisi ameshaanza kazi.
"Napenda kutoa wito kwa Wananchi tutuze mazingira ili tusikose maji na hatujalala tunahakikisha ndani ya saa chache watu wa baadhi ya maeneo watapata maji," Aliongeza mhandisi Luhemeja.
Waziri wa Maji mheshimiwa Jumaa Aweso akiwa na mafundi wa Dawasa ambao walikuwa wanafanya kazi ya kuchepusha maji kutoka katika bomba kuu la Ruvu chini eneo la Tegeta Wazo kwaajili ya kuyatawanya maji katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam
Mafundi wa Dawasa wakiendelea na kazi ya kuchepusha maji kutoka katika bomba kuu la Ruvu chini eneo la Tegeta Wazo kwa ajili ya kuyatawanya maji katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni