Torinto Hot media Blog.
Na Jerome Mlaki wa DAR.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa mapendekezo kwa serikali juu ya miswada ya maboresho ya Sheria mitatu iliyowasilishwa bungeni, ukiwemo wa msawada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote kutokana na kuwa na makosa katika baadhi ya vifungu.
Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga amesema umekuwepo na baadhi ya vifungu kuwa na mapungufu katika muswada ya Bima ya Afya kwa wote kwa kutoweka wazi sifa za kumtambua mtu huyo asiye na uwezo jambo linaloweza kuleta changamoto hapo baadaye.
"Baadhi ya vifungu walivyo na kasoro katika muswada ya Bima ya Afya kwa Wote ni pamoja na kifungu cha tatu kinachotoa tafsiri ya mtu asiye na uwezo bila kudadavua bayana ni yupi mtu huyo asiye na uwezo". Alisema Wakili Henga.
Alisema kifungu D 20 (1) katika mswada huo ambacho kimeweka takwa la lazima kwa mwajiri kuwasilisha jina la muajiriwa wake katika mfuko wa bima ya afya katika kipindi cha ndani ya siku 30 tangu kusaini nae mkataba.
Akitolea mfano kifungu cha 21 b ambacho kinampa mamlaka waziri wa afya kutunga kanuni zitakazoweka bima ya afya kuwa takwa la lazima kwa kila mtanzania.
LHRC tunashauri na kupendekeza kuwepo kwa kifungu ambacho kitaeleza mikakati ya serikali na namna ambavyo itakayowezesha kila mtanzania kuwa bima ya afya.
Aidha wakili Henga ameishauri serikali kupitia upya kifungu cha 32 kutolana na kumnyima haki mtanzania kupata baadhi ya huduma kama vile kitambulisho cha Utaifa, leseni ya Udereva, huduma za usajili wa laini na huduma nyingine.
“Tunatambua umuhimu wa kuwa Bima lakini kifungu hiki kitapelekea mtanzania kutokupata huduma mbalimbali muhimu,” Alisema wakili Henga
0 maoni:
Chapisha Maoni