TORINTO HOT BLOG.
Na..Jerome MLAKI
Watoto wakike wengi wamekuwa wakitumia njia ambazo sio salama za kujihifadhia wakati wa hedhi na hii imedhihilika hasa kwa maeneo ya vijijini kwani wengi utumia vipande vya kanga na wengine utumia hata ugali kujihifadhi wakiwa katika siku zao.
Afisa Program Msaidizi wa Utafiti, Taarifa na Uchambuzi Ndugu Jackson Malagalila akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es salaam
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Afisa Program Msaidizi wa Utafiti, Taarifa na Uchambuzi Ndugu Jackson Malagalila alipokuwa akiongea na waandhishi wa habari katika mfurulizo wa semina za jinsia na maendeleo zinazofanyika kila jumaa tano Makao Makuu ya TGNP Mtandao.
Afisa huyo alisema kuwa kwa sasa wapo katika kampeni kabambe ya kuhamasisha mpango wa hedhi salama kwa watoto wa kike, ambapo zoezi hilo lilianza rasmi tangu tarehe 28 mwezi mei mwaka huu ambapo ilikuwa ni kilele cha maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani.
Aliendelea kusema kuwa lengo kuu la semina hii ni kujadiliana kwa pamoja na wananchi kuhusiana na nafasi ya bajeti katika upatikanaji wa hedhi salama kwa watoto wa kike, na hii ikienda sambamba na uwepo wa matundu ya vyoo ya kutosha na vyumba vya kujihifadhia kwa watoto wa kike wawapo mashuleni.
Mshiriki wa semina za Jinsia na maendeleo Dada Nyanjura Kalindo akitoa maoni yake kuhusiana na nafasi ya Bajeti Kuu katika kufanikisha swala la Hedhi salama kwa watoto wa kike.
“Lakini pia kampeni hii inaanza katika ngazi ya familia katika kumkumbusha Baba au Mlezi kuwa katika bajeti unayotoa kwa watoto wako wakike na wakiume basi unatakiwa kuzidisha kidogo kwa mtoto wa kike ili aweze kupata mahitaji yake muhimu na ya lazima wakati akiwa katika siku zake”.alisema Afisa Jackson
Ndugu Jacksoni alisisitiza kuwa hii pia ni nafasi ya serikali kuweza kujitathmini kuwa inafanya jitihada gani kuhakikisha mabinti hawa wanapatiwa taulo za kujihifadhia kwa kuweza kutenga bajeti itakayowakomboa mabinti hawa kwa kuiga mfano kwa majirani zetu wakenya kwa mwaka 2016 Rais Uhuru Kenyata aliweka saini na mpango ukapita na mpaka sasa zoezi hilo linafanyika nchini humo.
Mzee Hamisi Masanja akitoa maoni yake kuhusiana na swala la wazazi wa kiume kushiriki katika kuwapatia watoto wao wakike taulo za kujihifadhia.
Kwa upande wake Mzee Hamisi Masanja kutoka kata ya Manzese aliongezea kwa kusema kuwa cha muhimu ni wakina Mama kuvunja ukimya kwa kuweza kumwambia Baba ukweli ili aweze kuongeza fedha kidogo katika bajeti ya nyumbani kwa ajiri ya mtoto wa kike na mama yake kipindi wakiwa katika siku zao.
“Lakini pia kwa watoto wa kike nao kutokaa kimya na kuweza kuongea na wazazi ama walezi wao kuhusiana na hali halisi ilivyo kwa sasa kwani binti akishindwa kufanya hivyo na hali fedha anayopewa shuleni ni ndogo basi anajitengenezea mazingira ya kushawishiwa na vijana wakiume na hatimae kuharibiwa maisha”.alisema Mzee Masanja
Na mwisho alisema kuwa inabidi ifike kipindi tuachana na mila zetu za kiafrika na kuweza kuvunja ukimya kwa wazazi wa kike kuwaeleza wazazi wa kiume kuhusu swala la hedhi salama kwa watoto wao, lakini pia watoto wakike kuweza kuongea na wazazi wa kiume kuhusu swala la hedhi salama kwani sio kitu cha ajabu tena cha kumshangaza mwanaume yeyote.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.
0 maoni:
Chapisha Maoni