Na Jerome Mlaki
Picha Na Jerome Mlaki Dar es Salaam.
TIC yasajili miradi mpya 109 ya uwekezaji.
TIC yasajili miradi mpya 109 ya uwekezaji.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema katika kipindi cha miezi minne (Januari-Aprili) mwaka huu kimesajili miradi mipya 109 ya uwekezaji huku kikibainisha kukamilika kwa miradi hiyo kunatarajia kutoa fursa za ajira 18,172.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Geofrey Mwambe wakati anatoa mafanikio ya TIC katika kuipindi hicho huku akieleza uchumi wan chi unakua kwa kasi kubwa na kwa sasa nchi inashika nafasi ya tano kati ya mataifa 10 duniani ambayo uchumi wake unakua kwa kasi.
Amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk Magufuli iliyomstari wa mbele katika kupambana na rushwa, ufisadi, kuondoa urasimu na kutengeneza mazingira wezeshi ya usajili wa biashara na leseni kwa wawekezaji wa ndani na nje.
Amefafanua kuwa mambo mengine yaliyofanyika katika kuhakikiksha wawekezaji wanahudumiwa vizuri ni uboreshaji wa mfumo huduma mahala pamoja ndani ya TIC na kubainisha kwa sasa kuna maofisa zaidi ya 10 wanaotoka wizarani na taasisi za serikali kwa ajili ya kutoa huduma za kusajili kampuni.
Ameongeza kuwa maeneo ya miradi iliyosajiliwa ni sekta ya viwanda,usafirishaji, ujenzi, kilimo na majengo ya biashara na kwamba wawekezaji waliosajili miradi wanatoka nchi za ulaya na Asia.
Amewapongeza viongozi mbalimbali waliofanikisha usajili wakiwemo mawaziri, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Uhamsishaji wa Uwekezaji, John Mnali amesema changamoto zilizokuwa zinakikabili kituo hicho zinaendelea kufanyiwa kazi na serikali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, upatikanaji wa umeme wa uhakika na upatikanaji wa ardhi.
0 maoni:
Chapisha Maoni