NA Joseph Maiko
Vipodozi vilivyopigwa
mrufuku vyenye thamani ya milioni 72,406,500 pamoja na Pombe kali zilizopigwa
marufuku zenye thamani ya Milioni 11,356,000 vimekamatwa vikiwa kwenye maduka
mbali mbali kwa ajili ya kuuziwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo
Jijni Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA) ,Bi Agnes Kijo ,wakati wa alipokuwa anatoa taarifa kwa waandishi wa
Habari kuhusu ukaguzi maalum wa kukagua na kuondoa katika soko
vipodozi visivyosajiliwa,pombe kali zisizosajiliwa pamoja na kufuatilia uhalali
wa biashara ya vipodozi kwenye mitandao ya kijamii.
Ambapo, Bi Kijo
amesema katika Ukaguzi huo ambao ulishirikisha Jeshi la Polisi,TFDA,Shirika la
Viwango nchini (TBS),Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na Ofisi ya
Rais,
Amesema katika ukaguzi
huo ulifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam,Pwani,Mwanza,Shinyanga,Geita,Mara
na Arusha ambapo ukaguzi huo ulichukua mda wa siku mbili.
Bi Kijo amevitaja
vipodozi vilivyokamatwa ni Carolight cream,Citrolight Crem,Sivoclaire Cream,Max
light cream,dawa zinazodaiwa kuongeza maumbile kwa wanaume(Maxman capsules)
sabani za kurudisha usichana ( Virginity soap).
Vipodozi vengine
ni Dawa za kuongeza ukubwa wa maziwa kwa wanawake (Papaya breast enlarging
crem) pamoja na dawa za kutibu magonjwa ambazo zimekuwa zikitumika kimakosa.
Sanjari na Vipodozi
hivyo vilivyopigwa marufuku pia katika ukaguzi huo wamekatamata pombe
kali zenye ujazo milimita 200 ambazo zinazofungashwa kwenye viroba.
"Tumekamata pombe
hizi ni imperial blue whsky,White mischief vodka,contessa preimium dry gin
vodka,Konyagi (Ladha ya pesheni)magic movement vodka,officers choice ,Dewer's
white label,Officers can spirit,sinature vodk "amesema Bi Kijo.
Hata hivyo Bi Kijo
amesema baada ya ukaguzi huo wamechukua hatua mbali mbali ikiwemo kufunga
majadala 24 ya kesi katika vituo mbali mbali vya Polisi dhidi ya
watuhumiwa na majengo ya biashara 29 yamefungwa.
"Baada ya
uchunguzi wa makosa kukamilika hatua mbali mbali zinatachukuliwa ikiwa ni
pamoja kukamilika kwa hatua mbali zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na
kuwapeleka mhakamani watuhumiwa na kutoa dhabu kulingana na sheria ya
Chakula,Dawa na Vipodozi ,Sura 219"
"Adhabu hizo
zinajumuisha kufutwa leseni ya biashara na kuharibu bidhaa zilizokamatwa kwa
gharama ya mtuhimiwa"amesema
Bi Kijo amewataka
wananchi kuendendelea kutoa taarifa za wale wote wanaojihusisha na biashara ya
vipodozi vilivyopigwa marufuku ,Biashara harany ya vipodozi na dawa katika mitandao
ya kijamii ili hatua zichukuliwe na Mamlaka husika.
0 maoni:
Chapisha Maoni