Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ameeleza maneno ya mwisho aliyoambiwa na marehemu Kasuku Bilago aliyekuwa Mbunge wa Buyungu mkoani Kigoma, ambapo alimwambia anahitaji msaada wa haraka wa matibabu.
Akizungumza katika ibada fupi ya kuuaga mwili wa marehemu Bilago, Mbowe amesema wakati alipokuwa nje ya nchi, nchini Afrika Kusini Bilago alimtumia ujumbe kwamba hali yake kiafya si nzuri hivyo anahitaji msaada.
“Nilipokuwa safarini nchini Afrika Kusini, mwalimu Bilago aliniambia ninaumwa hivyo naomba ushauri, nikawasiliana na bunge kuhusu taarifa yake ndipo walipomuamishia muhimbilli.Mwalimu aliliona hilo kwamba alikuwa anahitaji msaada wa haraka wa matibabu na kunitumia ujumbe nikiwa Afrika Kusini,” amesema Mbowe na kuongeza;
“Ndipo nilifunga safari Ijumaa, Jumamosi nilienda Muhimbili, nilimkuta hali yake imebadilika ghafla akakata kauli, nikaonana na madaktari ili wafanye juhudi za makusudi lakini walijaribu kwa muda wa nusu saa lakini ilishindikana, mwenzetu alikuwa ashatutoka na kutangulia mbele ya haki.”
0 maoni:
Chapisha Maoni