Wakati serikali na vyombo mbali mbali vya haki za ninaadam zikipinga na kukemea vikali tabia ya kufanya unyanyasaj kwa watoto na kijinsia na ukiukwaji wa haki za binaadam lakini bado watu hawana uelewa na jambo hilo
Hayo yamedhihirika Leo ambapo habari 24 imeshuhudia Dada mmoja mkaazi wa chasimba Mtaa wa basihaya kinondoni jijini Dar es salaam kumpiga mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka kumi na mwanafunzi wa darasa lapili katika Shule ya msingi Boko,
Wakiongea na HABAR 24 majirani wa Dada huyo wamesema wamechoshwa kuna manyanyaso anayopata Agnes fhidi ya dadake na wameomba vyombo vya sheria kumchkulia hata Dada huyo kwani nimekuwa ni kawaida yake kumpiga Mtoto huyo na muda mwingine kumzuia mtoto kwenda Shule mpaka yeye atakapo maliza biashara zake za kuuza mboga mboga
Dada huyo alofahamika kwa jina la Winifrifa Alex amekanusha malalaamiko hayo na kusema "Mimi simchap sana namchapa anapokosea tu na kama hajanikosea simchap na kama leo nimemchapa sababu hajafua Nguo tu " na kusisitiza kuwa yeye hana hata yoyote
Jukwaa LA wanawake LA Mtaa huo hawakuwa nyuma kwani walifika eneo LA tukio na kumpeleka Dada huyo katika vyombo husika vya sheria
Ni vyema kumfundisha mtoto kwa njia salaam na sio kwa kumdhuru kwa kipigo au kumnyanyasa kwa namna yoyote kwani huo ni ukiukwaji wa haki za kibinaadam na ni uvunjifu wa sheria
0 maoni:
Chapisha Maoni