Na Raufa Mrope Utouh news.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi hapo kesho katika warsha ya utafiti wa uchumi iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti ya Repoa ambapo inalenga kuleta misingi ya uzalishaji wenye tija na ushindani katika mazingira na masoko yenye ushindani.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dkt.Donald Mmari amesema kuwa warsha hiyo itawashirikisha wanazuoni, watafiti, watunga sera, watekelezi na wasimamizi, wahisani, sekta binafsi na Taasisi zisizo za kiserikali.
Aidha amebainisha kuwa katika warsha hiyo wataweza kujadili safari ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani, ukiongozwa na viwanda pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
"pamoja na kushuhudia ukiaji mzuri Kwa uchumi wa Tanzania Kwa miaka 15 iliyopita ,tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa viwango vya tija katika sekta nyingi bado ziko chini",alisema.
Hata hivyo ameongeza kuwa Tanzania inao uwezo wa kujiweka katika nafasi kubwa zaidi katika uchumi wa dunia, Kwa kujenga uwezo wa ushindani.
Ifahamike kuwa warsha ya mwaka huu itakuwa ya 23 tangu Taasisi ya Repoa ilipoanza kuandaa warsha kuu kwa kila mwaka.
0 maoni:
Chapisha Maoni