Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Mauzo kwa wiki iliyoishia 11 Januari 2018 yalikuwa shilingi milioni 371 na wiki iliyoishia tarehe 19 Januari 2018 yakawa shilingi Bilioni 1.8.
Vile vile Idadi ya hisa zilizo uzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia tarehe 11 Januari 2018 zilikuwa hisa laki 7 na wiki iliyoishia tarehe 19 Januari 2018 idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa sokoni ilikuwa hisa milioni 1.96.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia tarehe 19 Jabuari 2018 ilikuwa kama ifuatavyo:
TBL……………………………………………67%
CRDB…………………………………………….17%
SWISS………………………………………………10%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 164 kutoka Shilingi Trilioni 22.7 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 22.9 wiki iliyoishia tarehe 19 Januari 2018. Ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei za hisa za DSE (12%), CRDB (9%), NMG (8%), na ACA (7%),
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 32 kutoka Trilioni 10.28 hadi kafika Shilingi Trilioni 10.3 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa ya DSE (12%) na CRDB (9%).
Kampuni
|
19 Januari 2018 (Shilingi)
|
11 Januari 2018 (Shilingi)
|
Badiliko (%)
| ||||
CRDB
|
9.38%
| ||||||
DCB
|
0.00%
| ||||||
DSE PLC
|
1,340
|
11.67%
| |||||
MBP
|
0.00%
| ||||||
MCB
|
0.00%
| ||||||
MKCB
|
-5.62%
| ||||||
MUCOBA
|
0.00%
| ||||||
NMB
|
2,750
|
0.00%
| |||||
PAL
|
0.00%
| ||||||
SWALA
|
0.00%
| ||||||
SWIS
|
3,500
|
-6.91%
| |||||
TBL
|
14,000
|
0.00%
| |||||
TCC
|
16,800
|
0.00%
| |||||
TCCL
|
1,200
|
0.00%
| |||||
TOL
|
0.00%
| ||||||
TPCC
|
1,460
|
0.00%
| |||||
TTP
|
0.00%
| ||||||
VODA
|
0.00%
| ||||||
YETU
|
0.00%
| ||||||
Kampuni zilirodhodheshwa kutokea Masoko mengine
| |||||||
ACA
|
5,860
|
6.74%
| |||||
EABL
|
5,180
|
-0.58%
| |||||
JHL
|
10,920
|
4.00%
| |||||
KA
|
-2.78%
| ||||||
KCB
|
0.00%
| ||||||
NMG
|
2,490
|
7.79%
| |||||
USL
|
-10.00%
| ||||||
Mtaji Jumla Makampuni yote (Bilioni)
|
22,892
|
0.72%
| |||||
Mtaji Jumla Makampuni ya Ndani (Bilioni)
|
10,319
|
0.31%
| |||||
Kiashiria cha DSEI (pointi)
|
2,377
|
0.72%
| |||||
Kiashiria cha TSI (pointi)
|
3,936
|
0.33%
|
Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimeshuka kwa pointi 17 kutoka pointi 2,360 hadi 2,377 pointi hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Dar es Salaam Stock Exchange Plc (DSE), CRDB Bank Plc, Acacia (ACA), National Media Group (NMG),
na Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 12 kutoka pointi 3,924 hadi pointi 3,936 kutokana na kupanda kwa bei za hisa za DSE, CRDB.
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 5,504
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa poniti 53 kutoka pointi 2463 kadi pointi 2517
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imeshuka kwa pointi 11 kutoka pointi 2473 hadi pointi 2,462 imechangiwa na kushuka kwa bei za hisa za Swissport kwa 7% kutoka shilingi 3760 hadi shilingi 3500
Hati Fungani (Bonds)
Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 19 Januari 2018 yalikuwa Shilingi milioni 522 kutoka Shilingi bilioni 45 wiki iliyopita ya 11 Januari 2018
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na tatu (13) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi milioni 590 kwa jumla ya gharama ya Shilingi milioni 522
0 maoni:
Chapisha Maoni