TUMAINI katika jamii inayoendelea muda wote, sikumbuki ni wakati gani kulikuwa hamna barabara zinajengwa, kila siku simu mpya zinatoka, mitandao ya jamii mipya kama Facebook, Twitter na sasa Instagram. Tunapenda vitu vizuri. Chakusikitisha, hili jambo la kupenda vitu vizuri limeingia katika mahusiano yetu na limesababisha michepuko.
Sijawahi kuona mwanaume anajipiga kifua mbele ya mwanaume wenzake na kujigamba kuwa yeye ni mwaminifu kwa mke au girlfriend wake. Mwanaume anayetembea na wanawake wengi ndio anaonekana mjanja kuliko wenzake. Chakusikitisha zaidi, hapa nyumbani Tanzania, michepuko ndio dili, wanawake wengi waliopo kwenye ndoa wamekubaliana na hali ya wanaume wao kuchepuka. Utakuta mtu umeolewa lakini kazi yako ni kuchungulia whatsapp ya mpenzi wake na kuwaonya wanawake wengine waachane na mume wako, hivi mwanaume kama huyo unabaki naye wanini? huogopi kuletewa magonjwa?.
Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa anampenda sana mke wake na ameamua kuwa siku ya Jumanne na Jumatano hatogusa mwamamke mwingine, ni siku spesho kwa mke wake tu. Na anaamini kwa moyo wake wote kuwa hamna kosa lolote analofanya, na ni haki yake kuchepua.
Shetani wa ngono ameivamia nchi yetu, kila mtu ninayemjua “at least ” ana mchepuko mmoja. Watu hawafikirii mambo ya maendelea zaidi ya michepuko. Mi nawaambia michepuko sio dili na inapoteza muda sana na kuturudisha nyuma kimaendeleo.
Angalia picha hapo chini utajionea maneno ambayo yametafutwa zaidi ‘Google’ (Google trends image search) mwaka 2014 kati ya nchi za Kenya, Uganda na Tanzania. Utaona maneno ambayo yametafutwa kwa wingi kwa mwaka huu, utajionea nini kimejaa vichwa vya wananchi wa mataifa hayo hasa Watanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni