![](https://pbs.twimg.com/profile_images/725608678120931328/TGgItrkg.jpg)
NA Joseph Lieme
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imethitisha Mkataba na Kampuni ya Mwamkinga Auction Mart & Brokers iliyopewa kazi kudhibiti uegeshaji wa magari katika maeneo yasiokuwa rasmi katika Manispaa ya Temeke na Kigamboni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, amesema kuwa jiji imefatilia kwa ukaribu utendaji wa kampuni hiyo kufatia malalamiko ya wananchi kuhusu kufanya kazi kinyume na mkataba.
Amesema kuwa Kampuni ya Mwakinga ilikuwa inafanya kazi kwa niaba ya Halmashauri na ilitakiwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia sheria, miongozo, maelekezo pamoja na taratibu.
Mhe. Mwita amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikisababisha uonevu, kero na usumbufu kwa wananchi.
Amesema kuwa baada uchuguzi wa kina imebainika kuwa imekuwa ikifanya kazi zake kwa kutozingatia matakwa yao kwa kukiuka mkataba.
Ameitaka kampuni hiyo kuondoka kwenye maeneo iliyopangiwa kufanya kazi na kuhakikisha imekabidhi mashine zote za kukusanyia mapato halmashauri zikiwa katika hali nzuri.
Amesema kuwa halmashauri zote za jiji la Dar es Salaam zinatakiwa kuwaelekeza mawakala wake wote wa ukusanyaji wa mapato kwa kuzingatia mikataba yao ya kazi tofatuti na hapo haitasita kusitisha mikataba ya ya kazi.
April 1 mwaka huu Kampuni ya jiji la Dar es Saalam iliingia Mkataba ili ifanye kazi hiyo kwa niaba ya halmashauri.
Kwa kutumia sheria ndogo ya Maegesho ya Magari (G.N. Na. 60 ya mwaka 1998 na G.N. Na 41 ya mwaka 2017), jiji ina majukumu ya kusimamia, kuboresha na kuendeleza maeneo ya maegesho katika jiji la Dar es Salaam.
Kupitia sheria hiyo halmashauri ya jiji ina mamlaka ya kuzuia uegeshaji wa magari sehemu zisizoruhusiwa, kudhibiti matumizi mabaya ya barabara bila kuzingatia taratibu na kusababisha usumbufu na msongamano katika mitaa.
0 maoni:
Chapisha Maoni